Abel, Asimwe
(2019)
Kuchunguza Athari za Kifonolojia za Lugha ya Kihaya Katika Kujifunza Lugha ya Kiswahili.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Tasnifu hii ilichunguza athari za kifonolojia za lugha ya Kihaya katika kujifunza lugha ya Kiswahili kwa jamii ya wazungumzaji wa lugha ya Kihaya katika wilaya ya Misenyi. Wataalamu wengi wanakubaliana kuwa lugha zinapokutana huwa zinaathiriana kwa namna moja au nyingine. Kwa hivyo utafiti huu ulichunguza athari za kifonolojia za lugha ya Kiswahili katika jamii ya Kihaya. Eneo lililohusika katika utafiti huu ni wilaya ya Missenyi, mkoani Kagera. Njia zilizotumika kuwapata watafitiwa ni usampulishaji makusudi na nasibu. Usampulishaji makusudi ulitumika kwa walimu wanaofundisha darasa la awali hadi darasa la tatu na walimu wakuu wa kila shule. Usampulishaji nasibu ulitumika kwa wanafunzi wote, walimu wanaofundisha darasa la nne hadi darasa sita, na wazazi wa vijiji husika. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia iliyoasisiwa na mwanaisimu Vennemann (1971) ingawa baadaye iliendelezwa na (Hooper, 1971). Nadharia hii imetumiwa ili kubaini namna lugha ya Kihaya ilivyoathiri lugha ya Kiswahili katika jamii ya Kihaya. Katika ukusanyaji wa data kutoka katika eneo la utafiti, mtafiti alitumia njia ya mahojiano na dodoso. Jumla ya watafitiwa 297 walihusika katika utafiti huu, kati yao wanafunzi walikuwa 239 sawa na asilimia 80.5% ya watafitiwa wote waliohusika, idadi nyingine ya 58 walikuwa walimu, na wazazi. Utafiti umeonesha kwamba, lugha ya awali ina nguvu ya kuathiri kifonolojia ya mtoto hata anapojifunza lugha ya pili. Ili kumsaidia mwanafunzi kujifunza lugha ya pili walimu na jamii nzima inabidi kushirikiana kwa karibu katika kumsaidia mwanafunzi kutamka maneno kwa lafudhi sahihi ya Kiswahili.
Actions (login required)
|
View Item |