Athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa

Mahimbo, Clotilda William (2019) Athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Mahimbo-TASNIFU- 9-07-2019.pdf] PDF
Download (545kB)

Abstract

Utafiti huu unahusu Athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa. Utafiti umeongozwa na nadharia ya Mofolojia Leksika. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka Wilaya ya Lushoto, kata ya Kwesimu. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa. Malengo mahsusi ya utafiti huu ni; Kubainisha mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa iliyoathiriwa na lugha nyingine; Kueleza athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa; Kubaini mambo yaliyosababisha Lugha nyingine kuathiri mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa. Mtafiti alitumia mbinu za hojaji na mahojiano katika ukusanyaji wa data. Sampuli ya watafitiwa 32 ilihusishwa kwa njia ya usampulishaji nasibu na usampulishaji kusudio, kwa kuzingatia kigezo cha umri, jinsia na elimu. Tafiti mbalimbali zilizofanywa katika kuchunguza vipengele mbalimbali katika sarufi ya lugha ya Kisambaa kwa ujumla si katika kuangalia athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kwamba mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa inaweza kuathiriwa na lugha nyingine zinazotumika pamoja . Pamoja na hayo vilevile utafiti huu umebainisha kuwa athari hazitokei kiholela zipo sababu/mambo yanayosababisha athari hizo kutokea na pia utafiti huu umebainisha mbinu za kutumia ili kukabiliana na athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 23 Sep 2021 09:21
Last Modified: 23 Sep 2021 09:21
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/3012

Actions (login required)

View Item View Item