Mahimbo, Clotilda William
(2019)
Athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu Athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya
Kisambaa. Utafiti umeongozwa na nadharia ya Mofolojia Leksika. Data za utafiti
huu zilikusanywa kutoka Wilaya ya Lushoto, kata ya Kwesimu. Lengo kuu la utafiti
huu ni kuchunguza athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya
Kisambaa. Malengo mahsusi ya utafiti huu ni; Kubainisha mizizi ya maneno ya
lugha ya Kisambaa iliyoathiriwa na lugha nyingine; Kueleza athari za lugha nyingine
kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa; Kubaini mambo yaliyosababisha
Lugha nyingine kuathiri mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa.
Mtafiti alitumia mbinu za hojaji na mahojiano katika ukusanyaji wa data. Sampuli ya
watafitiwa 32 ilihusishwa kwa njia ya usampulishaji nasibu na usampulishaji
kusudio, kwa kuzingatia kigezo cha umri, jinsia na elimu. Tafiti mbalimbali
zilizofanywa katika kuchunguza vipengele mbalimbali katika sarufi ya lugha ya
Kisambaa kwa ujumla si katika kuangalia athari za lugha nyingine kwenye mizizi ya
maneno ya lugha ya Kisambaa. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kwamba
mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa inaweza kuathiriwa na lugha nyingine
zinazotumika pamoja . Pamoja na hayo vilevile utafiti huu umebainisha kuwa athari
hazitokei kiholela zipo sababu/mambo yanayosababisha athari hizo kutokea na pia
utafiti huu umebainisha mbinu za kutumia ili kukabiliana na athari za lugha nyingine
kwenye mizizi ya maneno ya lugha ya Kisambaa.
Actions (login required)
|
View Item |