Matumizi ya maneno ya Biblia katika riwaya ya Rosa Mistika na Gamba la Nyoka”za Euphrase Kezilahabi

Mayo, Fernandes Francis (2020) Matumizi ya maneno ya Biblia katika riwaya ya Rosa Mistika na Gamba la Nyoka”za Euphrase Kezilahabi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of FERNANDES FRANCIS FINAL SUBMISSION.pdf] PDF
Download (325kB)

Abstract

Utafiti huu unahusu matumizi ya maneno ya Biblia katika riwaya ya Rosa Mistika na Gamba la Nyoka. Utafiti huu umeongozwa na malengo matatu ambayo ni kubainisha maneno ya Biblia katika riwaya ya Rosa Mistika na Gamba la Nyoka, kueleza dhima za matumizi ya maneno hayo na kubaini athari za matumizi ya maneno ya Biblia kwa Wakristo ukiongozwa na nadharia ya Uhemenitiki. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya upekuzi matini nakuwasilishwa kwa kutumia mkabala wa kiidadi na kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwepo kwa matumizi ya maneno ya Biblia katika riwaya hizo kama vile Kunyweni hii ndio damu yangu, Maskini wa roho, Kuungama dhambi, Kiti cha enzi, Utakatifu, Damu yao na iwe juu ya vichwa vyenu mimi ninanawa mikono kama Pilato, Baba ikiwezekana kikombe hiki kinipite, Kwa jina la Baba, na Mwana na la Roho Mtakatifu, na Maria, mama wa Mungu aliyezaa kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Aidha, zipo dhima mbalimbali zilizojitokeza kama vile kulea watu kiroho, kukejeli, kufariji watu waliokata tamaa na kuonesha unafiki wa viongozi wa dini.Halikadhalika, zipo athari ambazo zimeonekana ambazo ni kutokuwa na imani na viongozi wa dini pamoja na kurudisha maendeleo nyuma. Kutokana na matokeo ya utafiti huu tunapendekeza kwamba, utafiti mwingine unaweza kufanywa kwa kuangalia matumizi ya maneno ya Biblia katika tanzu nyingine za fasihi kama vile tamthiliya, ushairi pamoja na fasihi simulizi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 22 Sep 2021 10:20
Last Modified: 22 Sep 2021 10:20
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2951

Actions (login required)

View Item View Item