Mayo, Fernandes Francis
(2020)
Matumizi ya
maneno ya Biblia katika riwaya ya Rosa Mistika na Gamba la Nyoka”za Euphrase
Kezilahabi.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu matumizi ya maneno ya Biblia katika riwaya ya Rosa Mistika na
Gamba la Nyoka. Utafiti huu umeongozwa na malengo matatu ambayo ni kubainisha
maneno ya Biblia katika riwaya ya Rosa Mistika na Gamba la Nyoka, kueleza dhima
za matumizi ya maneno hayo na kubaini athari za matumizi ya maneno ya Biblia kwa
Wakristo ukiongozwa na nadharia ya Uhemenitiki. Data zilikusanywa kwa kutumia
mbinu ya upekuzi matini nakuwasilishwa kwa kutumia mkabala wa kiidadi na
kimaelezo. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwepo kwa matumizi ya maneno ya
Biblia katika riwaya hizo kama vile Kunyweni hii ndio damu yangu, Maskini wa
roho, Kuungama dhambi, Kiti cha enzi, Utakatifu, Damu yao na iwe juu ya vichwa
vyenu mimi ninanawa mikono kama Pilato, Baba ikiwezekana kikombe hiki kinipite,
Kwa jina la Baba, na Mwana na la Roho Mtakatifu, na Maria, mama wa Mungu
aliyezaa kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Aidha, zipo dhima mbalimbali zilizojitokeza
kama vile kulea watu kiroho, kukejeli, kufariji watu waliokata tamaa na kuonesha
unafiki wa viongozi wa dini.Halikadhalika, zipo athari ambazo zimeonekana ambazo
ni kutokuwa na imani na viongozi wa dini pamoja na kurudisha maendeleo nyuma.
Kutokana na matokeo ya utafiti huu tunapendekeza kwamba, utafiti mwingine
unaweza kufanywa kwa kuangalia matumizi ya maneno ya Biblia katika tanzu
nyingine za fasihi kama vile tamthiliya, ushairi pamoja na fasihi simulizi.
Actions (login required)
|
View Item |