Tofauti za Msamiati baina ya Kiswahili cha Micheweni na Kiswahili Sanifu

Hamad, Tarehe khamis (2018) Tofauti za Msamiati baina ya Kiswahili cha Micheweni na Kiswahili Sanifu. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA TAREHE KHAMIS HAMAD.pdf] PDF
Download (774kB)

Abstract

Utafiti huu umelenga kuchunguza uhusiano uliopo baina ya tofauti za misamiati ya lahaja za Kipemba na zile za Kiswahili sanifu na jinsi tofauti hizo zinavyosababisha kukosekana kwa mawasiliano fanisi baina ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Utafiti huu umetumia muundo wa kimaelezo na majedwali, sampuli iliyotumika ni sampuli rahisi. Eneo la utafiti ni Mkoa wa Kaskazini Pemba Wilaya ya Micheweni. Mbinu zilizotumika kukusanya data ni dodoso, usaili pamoja na mahojiano, kigezo cha umri na ukaazi kilizingatiwa kwa watoa taarifa. Nadharia ya isimu linganishi ndiyo iliyotumika katika kuchambua data iliyokusanywa. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kwamba kuna tofauti kubwa ya misamiati ya kilimo na misamiati inayotumika katika mazingira ya nyumbani kati ya lahaja ya Kipemba na Kiswahili sanifu hasa katika matamshi. Matokeo hayo yamedhihirisha kuwa ingawa kuna tofauti hizo, pia kuna uhusiano wa karibu wa maana ya misamiati hiyo yenye tofauti za matamshi na maumbo. Aidha matokeo hayo yamedhihirisha pia kwamba kwa kiasi fulani hali hiyo imesabababisha kukosekana mawasiliano fanisi baina ya wazungumzaji inayojitokeza kwa wazungumzaji wa Kiswahili cha Micheweni na wazungumzaji wa Kiswahili Sanifu. Mwisho utafiti huu unapendekeza kuwa wale wenye nia ya kuandika kuhusu isimu ya Kiswahili kwa kuchunguza maneno ya maeneo mbali mbaliya maeneo ya Kaskazini mwa kisiwa cha Pemba watumie matokeo ya utafiti huu kama mwongozo utakaowasaidia kuandika tafiti zingine. Hata hivyo, walimu na wanafunzi watumie tasnifu hii kama rejea ya kupata msamiati unaotumika katika Ki-Micheweni na Ki-Sanifu. Hata hivyo taasisi mbali mbali za lugha zihifadhi katika maandishi maneno ya Ki-Micheeweni na kuonesha wasemaji wa Ki-Micheweni wanazungumza Kiswahili cha kale kinachotofautiana kimatamshi na Ki-Sanifi

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 11:58
Last Modified: 21 Sep 2021 11:58
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2918

Actions (login required)

View Item View Item