Ali, Maryam Rashid
(2018)
Athari za Utandawazi katika Lahaja ya Kipemba.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unalenga kuchunguza athari za utandawazi katika lahaja ya Kipemba.athari hizo ambazo zinaonekana kuendelea kukuwa siku hadi siku. Mtafiti wa utafiti huu aliongozwa na malengo mahsusi mawili ambayo na kuchunguza athari za utandawazi katika lahaja ya Kipemba. Kubainisha sababu zinazopelekea mabadiliko ya msamiati katika lahaja ya Kipemba. Utafiti huu umefanyika katika kisiwa cha Pemba mkoa wa kaskazini na kusini, na katika sehemu mbali mbali mjini na vijijini. Mbinu ya uwandani na muktadha zilitumika katika kufanya utafiti huu. Na njia zilizotumika ni dodoso, mahojiano na usomaji matini. Sampuli iliyotumika ni watoto, vijana na wazee, waliosoma na wasiosoma. Mtafiti aliongozwa na nadharia ya Fonolojia Zalishi Asili. Matokeo ya utafiti huu inaonyesha kwamba Lahaja ya kipemba imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na utandawazi. Pia, mtafiti amegundua kuwa yapo mabadiliko makubwa ya msamiati katika lahaja ya Kipemba. Pia mtafiti amegundua kuwa athari hizo zipo za aina mbili athari hasi na athari chanya zinazotokana na utandawazi.
Actions (login required)
|
View Item |