Ulinganifu wa Kiisimu kati ya Kitumbatu cha utumbatuni na Kibumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja

Amrani, Safia Burhan (2018) Ulinganifu wa Kiisimu kati ya Kitumbatu cha utumbatuni na Kibumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA SAFIA BURHAN AMRANI.pdf] PDF
Download (639kB)

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza tofauti za kiisimu, baina yaKitumbatu cha Utumbatuni na Kibumbwini mkoa wa kaskazini Unguja. Utafiti unaendeleza mbele hatua za kutafiti lahaja za Kiswahili pamoja na lugha ya Kiswahili kwa ujumla, ambapo kazi hii inatolewa mawazo katika maeneo hayo, na vijiji vya kaskazini kwa ujumla. Aidha katika kufikia lengo kuu la utafiti huu ulikuwa na malengo mahsusi yafuatayo: Kufafanua ulinganifu wa kimofolojia kati ya kitumbatu cha Utumbatuni na Kitumbatu cha Kibumbwini, kufafanua ulinganifu wa kimsamiati kati ya Kitumbatu cha Utumbatuni na Kitumbatu cha Kibumbwini na Kubainisha tofauti na uwiano wa kimaana kati ya Kitumbatu cha Utumbatuni na Kitumbatu cha Kibumbwini. Data za uwandani za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji pia sampuli lengwa na sampuli tajwa, zimetumika kuchagua watoa taarifa kwa vigezo vya umri na ukaazi. Vifaa kama vile karatasi na dodoso, zimetumika wakati wa kukusanya data. Nadharia ya muachano na makutano zimetumika kuchambua data. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa hakuna tofauti kubwa za kiisimu baina ya Kitumbatu cha Utumbatuni na Kibumbwini, katika vipengele vya mofolojia, msamiati na maana ambayo mtafiti amefanyia kazi. Kiswahili cha Kibumbwini kinaonekana kubeba baadhi ya msamiati iliyo egemea katika Kiswahili sanifu, na baadhi imeegemea katika lugha ya Kitumbatu, kwa upande wa mofolojia imeonekana tofauti ndogo katika maumbo ya njeo, nafsi, viwakilishi na kauli, vile vile katika maana imejitokeza tofauti zaidi katika vitenzi vya mjengoe.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 11:35
Last Modified: 21 Sep 2021 11:35
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2914

Actions (login required)

View Item View Item