Matumizi ya Lugha ya Ishara Katika Nyimbo za Taarabu: Uchunguzi wa Nyimbo za Mohamed Ahmed Moh’d

Ali, Asha Ramadhan (2018) Matumizi ya Lugha ya Ishara Katika Nyimbo za Taarabu: Uchunguzi wa Nyimbo za Mohamed Ahmed Moh’d. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA ASHA RAMADHANI ALI.pdf] PDF
Download (608kB)

Abstract

Mtunzi wa kazi ya fasihi ni mtu muhimu sana na kazi yake ya fasihi huwa ni jicho la jamii. Hivyo anaitumia sanaa yake ya utunzi kiubunifu zaidi katika kuyaeleza yale yanayoikumba jamii yake. Moja kati ya mbinu anazozitumia mtunzi wa kazi ya fasihi ni matumizi mazuri ya lugha ya ishara. Utafiti huu umelenga katika kuzibainisha ishara zilizotumika katika nyimbo za taarab asilia zilizotungwa na mtunzi Mohammed Ahmed Mohammed. Tasnifu hii imebainisha wazi jinsi ishara hizo zilivyojengwa kupitia nadharia ya Semiotiki, katika kuzieleza ishara hizo zilizomo katika utunzi wake, mtafiti ametumia nyimbo kadhaa zilizotungwa na msanii huyu alizozipata kupitia watafitiwa wake na nyengine alizozipata kutoka kwa mtunzi mwenyewe na kuzibainisha ishara hizo na dhima zake kwa maisha ya jamii ya sasa. Lengo kuu la utafiti huu ni kubainisha matumizi ya lugha ya ishara yaliyotumika katika nyimbo zilizotungwa na Mohammed Ahmed na kuzibainisha ishara hizo kwa kuzifafanua ili kujuwa makusudio ya nyimbo yenyewe na kuzielezea kiashiria cha ishara hizo na dhima zake kwa jamii ya sasa. Mada hii iliyoteuliwa kwa misingi kwamba kazi ya fasihi huibua maana ya kisemiotiki na kuwa nyimbo zilizopendekezwa hazijawahi kufanyiwa uhakiki wa ishara kwa mtazamo wa nadharia ya kisemeotiki, mfano wa nyimbo zilizofafanuliwa ni, kibiriti na petrol, Nanasi, Nampenda kumwambia siwezi, Kunguru, Kanikimbia, Nilikuchagua, Kisebusebu, Sikujuwa kama mapenzi matamu, Lishalo haliji tena, Kweli alikuwa wangu, Mpenzi wangu hawezi, Komamanga, Ndege wangu, Ndege karuka karudi. Tasnifu hii imejengwa na sura tano ambapo katika sura ya kwanza imepangiliwa na usuli wa mada, Kauli ya utafiti, Malengo ya utafiti, Umuhimu wa utafiti, Maswali ya utafiti na mipaka ya utafiti. Katika sura ya pili imepangwa kwa Mapitio ya kazi tangulizi, Fasihi na lugha, nadharia ya utafiti. Kwa upande wa sura ya tatu imejengwa kwa Mbinu za ukusanyaji wa data, usanifu wa utafiti eneo la utafiti, aina ya data zilizokusanywa, mbinu za kukusanyia data za upili, uchambuzi wa data, sampuli na usampulishaji. Sura ya nne inahusisha uchambuzi wa data za awali na za upili, ambao umejumuisha nyimbo zilizokusanywa na zilizofafanuliwa na watafitiwa. Sura ya mwisho imekamilisha kazi hii kwa kutoa matokeo ya utafiti huu ambayo yametoa aina ya ishara zilizopatikana katika nyimbo z

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 11:31
Last Modified: 21 Sep 2021 11:31
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2913

Actions (login required)

View Item View Item