Moh’d, Bishara Nassor
(2018)
Kuchunguza Viambishi Njeo na Hali katika Lahaja ya Kitumbatu.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Tasnifu hii ilihusu Uchunguzi wa Viambis injeo na Hali katika Lahaja ya Kitumbatu. Utafiti huu ulifanyika katika shehiya mbili za jimbo la Kiwani, shehia ya Mwambe na shehia ya Jombwe, katika vijiji vya Tasni, Bwegeza, Chanjani na Mwambe. Jumla ya watafitiwa 50 ya vijana na wazee walioishi Utumbatuni kwa muda mrefu walishiriki katika utafiti.Utafiti huu ulikuwa na malengo mahususi mawili; lengo la kwanza ni kubainisha viambishi njeo na hali katika lahaja ya Kitumbatu, na lengo la pili ni kuchanganua athari za kimofofonolojia zinazojitokeza katika vitenzi vya Kitumbatu wakati wa kudhihirisha viambishi njeo na hali. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya Dodoso, usaili na uchunguzi makini kisha kachambiliwa kwa kutumia mkabala usio wa kiidadi (maelezo) kwa kuongozwa na nadharia ya mofofonolojia ya Trubezkoy ya (1929). Matokeo ya utafiti yameonyesha kwamba njeo za nyakati na hali mbalimbali zilizojitokeza na michakato ya kimofofonolojia imedhihirishwa na mabadiliko ya miundo, kutoka muundo ndani kwenda miundo nje. Mabadiliko hayo yamedhihiri kupitia kanuni mbalimbali za kimofofonolojia kama vile udondoshaji, uyeyushaji na tangamano lairabu. Mtafiti amependekeza kuwa tafiti zijazo zijfanye utafiti zaidi juu ya uchambuzi wa kimofosintaksia za lahaja zifanyike, ili kubaini jinsi viambishi vya njeo vinavyoathiri vitenzi vya lahaja husika. Pili, mtafiti amependekeza kwamba tafiti nyingine za Kimofofonolojia zifanywe kwenye lugha za Kibantu ili kubaini kwa kiasi gani vitenzi vya Kibantu huathirika kutokana na michakato ya kimofofonolojia.
Actions (login required)
|
View Item |