Abdalla, Abdalla Juma
(2018)
Tofauti ya Rejista ya Makuli Wa Bandarini na Lugha Sanifu Ya Kiswahili.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Kazi hii inahusu kuchunguza tofauti ya rejista ya makuli wa bandarini Unguja na ya Kiswahili sanifu.Utafiti huu ulikuwa na malengo matatu ambayo ni . Kubainisha sifa za rejista yamakuli wa bandarini katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Kuchunguza sababu kuibuka kwa tofauti kati ya rejista hii na Kisawhili sanifu, na kubainisha athari zinazotokana narejista ya makuli wa bandarini na watumiaji wengine wa lugha ya Kiswahili. Ili kufikia lengo kuu lililokusudiwa, mbinu mbalimbali za utafiti zilihusika, ambazo ni hojaji, mahojiano pamoja na ushuhudiaji. Nadharia tatu zilitumika ambazo ni nadharia misimbo ya Bernstein,nadharia ya Giles ya maafikiano ambapo tumeangalia mazungumzo ya makuli wao wenyewe na wateja wao pamoja na nadharia ya vitendo usemi iliyoasisiwa na kuelezwa na mtaalamu Austin na Searle kwa kujikita katika mazungumzo baina ya makuli na wateja wao. Utafiti uligundua kwamba mazungumzo baina ya makuli na matajiri wao yamedhihirisha matumizi ya misimbo pana na misimbo finyu. Pia tumegunduwa kwamba kuna maafikiano baina ya makuli kama kikundi cha jamii kutokana na matumizi ya lugha yao. Mazungumzo baina ya makuli na matajiri wao yamedhihirisha kutokea kwa vitendo usemi ambavyo vinadhihirisha athari ya rejista ya makuli. Vile Vile utafiti umebaini kwamba usemi wa makuli wa bandarini umedhihirisha vitendo usemi ambavyo huwa na sifa ya kutambulika kutokana na kinachosemwa.Ili kutaka kujua athari ya kitendo fulani, sharti kuangalia kinachosemwa, kinasemwa wapi, na nani na kwa nani. Mtafiti amependekeza mambo kadha na kwa tafiti zijazo zitanue wigo na kufanyia kazi maeneo mengine Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na kufanya utafiti kwa kuangalia tofauti baina ya rejista ya makuli wa bandarini Unguja na rejista ya makuli wa bandari ya Dar salaama na kufanya utafiti baina ya makuli wanaobeba mizigo na makuli wanaobeba samaki bandarini feri Dar-salaam.
Actions (login required)
|
View Item |