Usawiri wa Mwanamme katika Riwaya ya Kiswahili: Joka La Mdimu na Watoto wa Mama Ntilie

Mohammed, Khamis Issa (2018) Usawiri wa Mwanamme katika Riwaya ya Kiswahili: Joka La Mdimu na Watoto wa Mama Ntilie. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU  YA KHAMIS ISSA MOHAMMED.pdf] PDF
Download (550kB)

Abstract

Mada ya utafiti huu ni Kuchunguza Usawiri wa mhusika mwanamme katika riwaya ya Kiswahili: Joka la Mdimu na Watoto wa Mama N‟tiliye. Malengo mahususi yalikuwa mawili ambayo ni kubainisha changamoto zinazomkabili mhusika mwanamme katika riwaya teule na kuelezea usawiri wa mhusika mwanamme kama unavyojitokeza katika riwaya teule. Sampuli ya utafiti huu ilikuwa ni riwaya mbili teule ambazo ziliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji lengwa. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa mwanamme katika riwaya teule anakabiliwa na changamoto za umasikini, rushwa, ulevi wa pombe na wanawake na kukosa uaminifu. Hivyo, kwa mapana zaidi usawiri wa mwanamme unaojitokeza katika riwaya teule ni kuwa mwanamme anasawiriwa kama mtu asiyefikiri bila kupata kilevi, asiyekuwa mwaminifu, mtu mwenye uelewa wa mambo, mtu mwenye huruma, mpumbavu, anayependa ugomvi, aliyelaaniwa, mfanyakazi ngumu, mtetezi wa wanawake, mtu asiyechoka wala kuona aibu, mbakaji na mnyanyasaji, asiyejiamini, anayedanganyika haraka, mwenye mapenzi kwa watoto na mtu asiyependa familia yake. Kwa jumla, imebainika kuwa mwanamme kama ilivyokuwa kwa mwanamke naye pia ana mambo mazuri anayoyafanya na kumpamba lakini pia anayo mambo mabaya ambayo kwa kawaida hapaswi kuwa nayo lakini kwa sababu ni binadamu hawezi kuyakwepa ni lazima yampate au ayafanye.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 10:30
Last Modified: 21 Sep 2021 10:30
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2905

Actions (login required)

View Item View Item