Mfumo Angami wa Kipemba na Athari zake katika Kuzuia Mawasiliano Fanisi kwa Wageni wa Lahaja hio

Mohammed, Aisha Ameir (2018) Mfumo Angami wa Kipemba na Athari zake katika Kuzuia Mawasiliano Fanisi kwa Wageni wa Lahaja hio. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA AISHA AMEIR MOHAMMED.pdf] PDF
Download (809kB)

Abstract

Utafiti huu unaohusu mfumo angami wa Kipemba na athari zake katika kuzuia mawasiliano fanisi kwa wageni wa lahaja hio, lengo lake kuu ni kuchambua mfumo angami katika lahaja ya Kipemba na jinsi mfumo huo unavyokwamisha mawasiliano kwa wageni wa lahaja ya Kipemba. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya viangama ya Zwicky (1977) amechambua aina tatu za viangama ambavyo ni viangama awali, viangama kati na viangama tamati pia utafiti umebaini kuwa kuna tatizo la kimawasiliano kwa wageni wa lahaja ya Kipemba kutokana mfumo angami wa Kipemba. Utafiti umetumia mbinu mbalimbali katika ukusanyaji wa data zake. Utafiti umefanyika Mwambe, Chokocho, Kiuyu mbuyuni naKwale. Walengwa wa utafiti huu ni wazee, watu wa makamo na vijana. Kila shehia wamesailiwa watu 20wa umri na jinsia tafauti na kufanyiwa usaili watu 80. Utafiti huu umetumia mbinu za hojaji, usaili na ushuhudiaji. Utafiti umetumia data simulizi ambapo mtafiti amefanya usaili na kushuhudia kwa kusikiliza mazungumzo kutoka mikusanyiko ya watu mbalimbali. Data zilichambuliwa kimaelezo. Kwa upande wa matokeo ya utafiti, data zimeonesha kuwa kuna aina tatu za viangama katika mfumo angami wa Kipemba ambavyo ni viangami awali, viangami kati na viangami tamati aidha data zinaonesha kuwa kunajitokeza tatizo la kimawasiliano kwa wageni wa lahaja ya Kipemba kutokana na mfumo angami wa Kipemba. Kwa upande wa mapendekezo mtafiti amependekeza ufanyike utafiti wa mfumo angami wa lahaja nyengine. Pia anapendekeza kufanyike utafiti wa kutofautisha na kufananisha mifumo angami ya lahaja mbali mbali.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 09:59
Last Modified: 21 Sep 2021 10:22
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2904

Actions (login required)

View Item View Item