Majina ya wanyama, ndege na wadudu jinsi yanavyoakisiwa na majina ya mitaa

Mohammed, Mwaka Mzee (2018) Majina ya wanyama, ndege na wadudu jinsi yanavyoakisiwa na majina ya mitaa. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA MWAKA MZEE MOHAMMED.pdf] PDF
Download (1MB)

Abstract

Utafiti huu ulizungumzia majina ya wanyama, ndege na wadudu jinsi yanvyoakisiwa na majina ya mitaa. Ulichunguza uhusiano uliopo baina ya majina ya wanyama, ndege na wadudu. Mtafiti aliongozwa na malengo matatu. Kwanza, kubainisha majina ya wanyama ndege na wadudu yanvyotumika kuwakilisha majina ya mitaa, pili, mahusiano ya maana ya majina ya mitaa na majina ya ndege, wanyama na wadudu na tatu, kuchambua sababu zinazochangia majina ya wanyama, ndege na wadudu kuakisiwa na majina ya mitaa. Ili kufikia lengo kuu lililokusudiwa mbinu mbali mbali za utafiti zilihusika. Mbinu hizo ni pamoja na mahojiano, ushuhudiaji pamoja na hojaji. Utafiti huu uliongozwa na nadharia jumuishi pamoja na nadharia ya semiotikiambazoziliakisi data za utafiti huu kutokana na maoni yaliyotolewa na watafitiwa na wanajamii kwa ujumla, ambapo maoni hayo yaliunda data za utafiti huu. Kwa upande wa matokeo ya utafiti, mtafiti aligundua kuwa majina ya mahali yana mfungamano na jamii na utamaduni wa jamii husika. Baadhi ya majina yanaakisi moja kwa moja shughuli za kiuchumi ama kijamii wanazofanya wanajamii. Hata hivyo, kuna majina ya mitaa ambayo hutokana na matendo ya kihistoria yaliyofanywa na wakazi wa maeneo hayo.Sambamba na hayo mtafiti katika kazi yake amegundua pengo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi, ambapo anapendekeza kufanyika kwa utafiti utaonesha athari za majina ya viumbe, vitu pamoja na matendo ya watu jinsi yanavyoakisi katika utoaji wa majina ya mitaa. Na pia athari za kifonojia, kimofolojia na kisemantikia vifanyiwe utafiti ili kuweza kuona jinsi gani wanajamii wanavyoweza kuvitawala vyema vipengele vya kiisimu katika utoaji na upangaji wa majina ya sehemu wanazoishi maishani.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 09:55
Last Modified: 21 Sep 2021 10:23
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2903

Actions (login required)

View Item View Item