Mchango wa Mazingira ya Kimaumbile katika Kuibua Majina ya Mahali Kisiwani Pemba

Hamza, Bimkubwa Abdulla (2019) Mchango wa Mazingira ya Kimaumbile katika Kuibua Majina ya Mahali Kisiwani Pemba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA BIMKUBWA ABDULLA HAMZA.pdf] PDF
Download (629kB)

Abstract

Kazi hii ilihusika na Kuchunguza Mchango wa Mazingira ya Kimaumbile katika Kuibua Majina ya Mahali Kisiwani Pemba. Utafiti huu ulikuwa na malengo mawili ambayo ni kubainisha majina ya mahali yanayotokana na mazingira ya kimaumbile yanayochangia upatikanaji wa majina ya mahali kisiwani Pemba na kuchunguza historia ya mazingira ya kimaumbile katika kuibua majina ya mahali kwenye sehemu mbalimbali katika kisiwa cha Pemba. Ili kufikia lengo kuu lililokusudiwa mbinu mbalimbali za utafiti zilihusika, ambazo ni hojaji na mahojiano. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni nadharia jumuishi ya Giles ambayo msingi wake mkubwa ni kuchunguza vibainishi vya jamii mbalimbali. Sampuli iliyotumika ni watu themanini na moja (81), kutoka maeneo mbalimbali ya Pemba. Kwa upande wa matokeo ya utafiti, aligundua kwamba mtafiti alibaini kuwa kisiwni Pemba yapo majina mengi yaliyotokana na mazingira ya kimaumbile kisiwni hapa. Mazingira ya kimaumbile yaliyochangia majina hayo ni miti mikubwa, milima, hali ya ardhi, mito, maziwa, shughuli za kibinaadamu kama mava, mabonde, mawe, na maumbile mengine. Kuhusu lengo la pili, mtafiti amegundua asili na historia ya majina hayo, na jinsi yalivyoibua majina ya mwahali humo. Alibaini shughuli kama uvuvi, usafiri, kilimo, ugomvi, mapumziko, uchotaji maji mitoni na pirika nyengine zilitoa umashuhuri wa mwahali humo na kufanya watu waamue kuyaita majina ya mahali kutegemeana na mazingira ya mahali hapo. Amebaini pia baadhi ya asili changizi zilizoibua majina zimetoweka na nyigine zinalindwa na kuhifadhiwa. Nyengine zimehifadhika kimaumbile na nyengine zimehifadhiwa kwa jitihada maalum za kijamii.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 09:45
Last Modified: 21 Sep 2021 09:45
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2902

Actions (login required)

View Item View Item