Ismail, Fatma Hassan
(2019)
Kuchunguza Mtindo na Dhamira katika Tamthiliya ya Mondlane na Samora.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu ni Kuchunguza Mtindo na Dhamira katika tamthiliya ya
Mondlane na Samora. Utafiti huu ulikuwa na malengo mahsusi mawili ambayo ni,
kubainisha vipengele vya mtindo katika tamthiliya ya Mondlane na Samora, na
kubainisha dhamira katika tamthiliya ya Mondlane na Samora
Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi wa madhumuni
maalumu. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya maktabani kwa njia ya usomaji
makini. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kutumia mbinu ya mkabala wa
kimaelezo. Aidha, nadharia ya Umitindo ilitumika kwa lengo mahsusi la kwanza,
sambamba na swali la utafiti la kwanza. Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji ilitumika
kwa lengo mahsusi la pili pamoja na swali la utafiti la pili. Nadharia zote hizo
zilifanikisha vyema kazi yakukusanya, kuchambua na kuwasilisha data za utafiti.
Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwatamthiliya ya Mondlane na Samora
imetumia vipengele vya mtindo vinavyohusu matumizi ya lugha na vile vinavyohusu
sajili mbali mbali kama vile barua, matangazo ya redio, mawasiliano ya simu na
lugha ya shuleni na jeshini. Dhamira zilizojitokeza ni ukoloni, harakati za kupigania
uhuru, umoja wa Bara la Afrika, umuhimu wa elimu, vita na mauaji, mapenzi na
ndoa. Dhamira zote zililenga kusawiri uhalisia wa maisha ya bara la Afrika wakati
wa ukoloni na wakati wa harakati za kutafuta uhuru kutoka kwa wakoloni. Mtafiti
amegundua kuwa Emmanuel Mbogo amekuwa akichota matukio ya kihistoria katika
jamii za Afrika kama msingi wa matumizi ya mitindo yake na dhamira zake katika
tamthiliya anazozitunga.
Actions (login required)
|
View Item |