Kuchunguza Dhamira za Mapenzi na Usaliti katika Riwaya ya Mfadhili

Moh`d, Fatma Rashid (2019) Kuchunguza Dhamira za Mapenzi na Usaliti katika Riwaya ya Mfadhili. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU YA FATMA RASHID MOH’D.pdf] PDF
Download (73kB)

Abstract

Utafiti huu unahusu Kuchunguza Dhamira za Mapenzi na Usaliti katika Riwaya ya Mfadhili. Lengo kuu ni kuchunguza dhamira za mapenzi na usaliti katika riwaya ya Mfadhili ya Hussein Tuwa. Utafiti huu umehusisha malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha dhamira za mapenzi zilizojitokeza katika riwaya ya Mfadhili. Lengo la pili ni kubainisha dhamira za usaliti zilizojitokeza katika riwaya ya Mfadhili na lengo la tatu ni kubainisha mbinu za kisanaa zilivyoibua dhamira za mapenzi na usaliti katika riwaya ya Mfadhili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mwitiko wa Msomaji katika lengo la kwanza la kwanza na la pili sambamba na suali la kwanza na la pili na nadharia ya Simiotiki katika lengo la tatu na suala la tatu. Mbinu iliyotumika kukusanyia data ilikuwa ni mbinu ya usomaji makini pamoja na upitiaji wa nyaraka maktabaniambapo mtafiti aliisoma kwa kina riwaya teule huku akidondoa data ambazo hatimae zilijibu maswali ya utafiti huu. Data za utafiti huu zilichambuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo. Aidha, utafiti huu uliongozwa na maswali matatu ya utafiti ambapo swali la kwanza lilikuwa ni; Ni dhamira zipi za mapenzi zilizojitokeza katika riwaya ya Mfadhili? Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa riwaya teule ya Mfadhili imeonesha mapenzi ya dhati ambayo ni kati ya baba na mtoto wake wa kambo, mtu na rafiki yake, mapenzi kati ya mtu na mchumba wake, mapenzi katika ndoa, mapenzi kati ya mtu na wifi yake, mapenzi kati ya daktari na jamii na mapenzi ya dhati kati ya mkuu wa kazi na wafanyakazi wake. Kwa upande mwengine kuna mapenzi ya uongo ambayo yamejitokeza kati ya mke na mume wake wa ndoa, mapenzi ya uongo kati ya mtu na mchumba wake na mapenzi ya uongo kati ya marafiki. Swali la pili lililoongoza utafiti huu lilikuwa; Ni dhamira zipi za usaliti zilizojitokeza katika riwaya ya Mfadhili? Data za utafiti zilionesha kwamba dhamira ya usaliti imejitokeza katika ndoa, usaliti katika mtu na mchumba wake, usaliti kati ya marafiki na usaliti unaofanywa watumishi wa umma na usaliti unaofanywa na wafanyakazi wa afya. Swali la tatu lililoongoza utafiti huu lilikuwa; Ni mbinu zipi za kisanaa zinazoibua dhamira za mapenzi na usaliti katika riwaya ya Mfadhili? Data za utafiti zilionesha kwamba dhamira ya mapenzi na usaliti zimeibulia kupitia vipengele vya lugha, wahusika na mandhari.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 800 Literature > 800 Literature, rhetoric & criticism
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 21 Sep 2021 08:39
Last Modified: 21 Sep 2021 08:39
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2897

Actions (login required)

View Item View Item