Abdulla, Juma Hamad
(2019)
Kuchunguza Usihiri katika Ngano za Zanzibar.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza usihiri katika ngano za Zanzibar. Utafiti ulijikita
kuchunguza namna vipengele vya usihiri vinavyojidhihirisha katika ngano za
Zanzibar na namna vipengele vya usihiri vilivyotumika kuibua dhamira katika ngano
teuele. Mtafiti alichagua mada hii kwasababu matumizi ya usihiri alibaini
hayajachunguzwa katika ngano za Zanzibar.
Utafiti huu ulifanyika uwandani katika ukusanyaji wa data. Maeneo yaliyotumika
kukusanya data ni Sizini, Micheweni, na Wingwi. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa
kwa kutumia mbinu ya madhumuni maalum. Aidha, data za utafiti huu
zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya maelezo. Utafiti huu uliongozwa na nadharia
ya Uhalisiajabu.
Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa ngano za Zanzibar zinatumia usihiri katika
vipengele vya ujenzi wa wahusika, ujenzi wa mandhari, motifu za safari, ndoto,
vyakula,wahusika, matukio mbali mbali Pia utafiti umegundua kuwa vipengele vya
usihiri katika ngano za Zanzibar vimetumika kuibua dhamira za ujasiri, malezi,
ushujaa, uongozi mbaya, utu, uchoyo, kiburi, uvivu, ukarimu, ujanja, nafasi ya
mwanamke, uhalifu, ukoloni na umaskini.
Actions (login required)
|
View Item |