Kutathmini Mtindo na Dhamira katika Riwaya za Eupharase Kezilahabi na Mohamed Suleiman: Utafiti Linganishi.

Ali, Amour Rashid (2020) Kutathmini Mtindo na Dhamira katika Riwaya za Eupharase Kezilahabi na Mohamed Suleiman: Utafiti Linganishi. ["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined] thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA AMOUR FINAL-09-12-2020.docx] PDF - Submitted Version
Download (1MB)

Abstract

Utafiti huu umeshughulikia mada iliyohusu ‘Kutathmini Mtindo na Dhamira katika Riwaya za Eupharase Kezilahabi na Mohamed Suleiman: Utafiti Linganishi" kwa kurejelea riwaya za Kichwamaji na Dunia Uwanja wa Fujo za Euphrase Kezilahabi na zile za Kiu na Nyota ya Rehema za Mohamed Suleiman”. Ili kutimiza kusudi hilo tulikuwa na malengo mahsusi manne; kubainisha mbinu za kimtindo katika riwaya teule za Euphrase Kezilahabi na Mohamed Suleiman, Kulinganisha mbinu za kimtindo katika riwaya teule za Euphrase Kezilahabi na Mohamed Suleiman, Kulinganua mbinu za kimtindo katika riwaya teule za Euphrase Kezilahabi na Mohamed Suleiman, na Kulinganua dhamira zinazojitokeza katika riwaya teule za Euphrase Kezilahabi na Mohamed Suleiman. Sampuli ya utafiti huu imeteuliwa kwa kutumia mbinu ya madhumuni maalumu. Data za msingi zilikusanywa kwa mbinu ya usomaji makini na kuchambuliwa kwa mkabala wa kimaelezo. Mjadala wa data uliongozwa na nadharia za teule Mwingilianomatini, nadharia ya Umitindo na Nadharia ya Umuundo. Utafiti umegundua kuwa waandishi wanatofautiana na kufanana katika mbinu za kimtindo na dhamira zilizotumika kujenga kazi zao za sanaa. Wasanii wote wanafanana katika vipengele vya matumizi ya methali, misemo, tashibiha, sitiari, tashihisi, nidaa, mchanganyo ndimi, mdokezo, mjalizo, matumizi ya barua, nyimbo, ndoto, nafsi, masimulizi, motifu za safari, majina sadfa ya wahusika na dayalojia. Pia, wanatofautiana katika matumizi ya mitindo, hasa ile ya oksimora, tabdila, mazida, udondoshaji, haipofora, nakadhalika. Kwa upande wa dhamira wametofautiana kuhusu zile zinazohusu maisha, uongozi, mapinduzi na kisasi, mapenzi na ndoa, ujirani na uhusiano na utamaduni. Maneno makuu: Umitindo, umuundo, mwingiliano mahiri, udondoshaji.

Item Type: Thesis (["eprint_fieldopt_thesis_type_phd" not defined])
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Mugisha Kafuma
Date Deposited: 07 May 2021 10:23
Last Modified: 07 May 2021 10:23
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2862

Actions (login required)

View Item View Item