Athari za Kikurya Katika Ujifunzaji wa Kiswahili Sanifu Miongoni mwa Wakurya

Gekondo, Janeth Maheri (2019) Athari za Kikurya Katika Ujifunzaji wa Kiswahili Sanifu Miongoni mwa Wakurya. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of JANETH MAHERI -TASINIFU-12-11-2019.pdf] PDF
Download (935kB)

Abstract

Utafiti huu ulihusu athari za Kikurya katika ujifunzaji wa Kiswahili Sanifu miongoni mwa Wakurya. Uliongozwa na malengo makuu mawili. Lengo la kwanza lilikuwa ni kuonesha jinsi gani maneno ya lugha ya Kikurya yanaathiri ujifunzaji wa Kiswahili Sanifu. Na, lengo la pili lilihusiana na kubainisha sababu zinazohangia athari za Kikurya katika kujifunza Kiswahili Sanifu. Ili kukamilisha azma ya utafiti kama ilivyokusudiwa, mbinu za hojaji na mahojiano zilitumika katika kukusanya data. Kadhalika utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Fonolojia Zalishi Asilia ambayo huchunguza bayana athari hizo za lugha ya kwanza (Kikurya) katika kujifunza lugha ya pili yaani Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa katika wilaya ya Tarime ambayo ilichukuliwa sampuli kati ya wilaya za Butiama na Serengeti zenye wakazi wengi ambao wanatumia lugha ya Kikurya kama lugha yao ya kwanza mkoani Mara. Katika uchanganuzi wa data matokeo yalionesha kwa kina jinsi ambavyo lugha ya Kikurya imeathiri lugha ya Kiswahili sanifu hususani katika vipengele vya matamshi (fonolojia), mofolojia pamoja na tahajia (uandishi) ambavyo mtafiti alivichunguza. Pia matokeo ya uchanganuzi wa data yalionesha kuwa; athari za lugha ya kwanza, mitazamo finyu katika jamii na kukosekana kwa baadhi ya sauti katika lugha ya Kikurya ni sababu zilizochangia lugha ya Kiswahili kuathiriwa. Aidha, baada ya kubaini changamoto zinazohangia athari hizo kuwepo, utafiti huu umetoa mapendekezo ya kuweza kusaidia kuzuia athari hizo katika jamii hasa kwa wakazi wanaoishi maeneo ya vijini. Jamii inapaswa kuelimishwa thamani ya lugha ya Kiswahili ili iweze kuondokana na mitazamo potofu juu ya lugha ya Kiswahili. Kwa kufanya hivi tutakuwa tumesaidia wanajamii kuipenda lugha ya Kiswahili na hivyo itawasababisha wajifunze lugha ya Kiswahili kwa ufasaha na pia kuizungumza kwa ufasaha.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 09 Dec 2020 13:24
Last Modified: 09 Dec 2020 13:24
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2607

Actions (login required)

View Item View Item