Uchunguzi wa Kisemantiki wa Majina ya Asili Katika Koo za Ginantuzu

Masanja, Njana Tegisi (2019) Uchunguzi wa Kisemantiki wa Majina ya Asili Katika Koo za Ginantuzu. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of MASANJA PhD FINAL NOV.2019.pdf] PDF
Download (2MB)

Abstract

Utafiti huu unahusu Uchunguzi wa Kisemantiki wa Majina ya Asili Katika Koo za Ginantuzu. Utafiti ulilenga: kuainisha majina ya asili; kuonesha vigezo vinavyotumika katika kuteua majina ya asili na kubainisha miktadha ya majina ya asili katika koo za Ginantuzu. Nadharia ya Uumbaji iliyoasisiwa na Sapir (1958) ndiyo iliyotumika kuongoza utafiti huu. Data za utafiti zilikusanywa katika mkoa wa Simiyu, wilaya ya Bariadi na Itilima. Jumla ya kata sita zilifanyiwa utafiti. Miongoni mwa kata hizo, vijiji kumi vilipitiwa na mtafiti. Jumla ya watafitiwa 80 walihusika katika kutoa taarifa zilizohusiana na mada ya utafiti. Watafitiwa hao walichaguliwa kwa kutumia usampulishaji nasibu na usampulishaji usio nasibu. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya hojaji na mahojiano. Katika kuchambua na kuwasilisha data, utafiti kwa kiasi kikubwa ulitumia mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa, majina ya asili katika koo za Ginantuzu yamewekwa katika makundi kumi na saba. Makundi hayo ni majina yanayotokana na wanyama, vitendea kazi, mazao, vyakula, matukio, mahali pa kuzaliwa, tabia na matendo, jinsi mtoto alivyozaliwa, na matunda. Makundi mengine ni majina yanayotokana na utani, vitu, ukoo, mimea, mfuatano wa watoto, itikadi ya dini na utawala, ujio wa vitu vipya na unasibu. Utafiti pia umebaini kuwepo kwa vigezo 10 vilivyotumika katika kuteua majina ya asili katika koo za Ginantuzu. Vigezo hivyo ni kigezo cha mazingira, utani, matukio yanayotokea, mahusiano katika familia, urithi, tabia na matendo, uchumi wa familia, ujio wa vitu vipya, mfuatano wa watoto na itikadi ya dini. Na mwisho utafiti umebaini kuwepo kwa miktadha 7 ya majina ya asili katika koo za Ginantuzu. Miktadha hiyo ni muktadha unaodokeza ukubwa, udogo, uzuri, udunishaji, uhusiano katika familia, mazoea, na tabia na matendo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr. Administrator OUT
Date Deposited: 04 Dec 2020 09:12
Last Modified: 04 Dec 2020 09:12
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2551

Actions (login required)

View Item View Item