Mchango wa Nyimbo za Michezo ya Watoto Katika Kukuza Maadili ya Jamii ya Wapemba,

Nassor,, Riziki Omar (2016) Mchango wa Nyimbo za Michezo ya Watoto Katika Kukuza Maadili ya Jamii ya Wapemba,. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of RIZIKI TASNIFU MATENGENEZO.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (954kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unachunguza Mchango wa Nyimbo za Michezo ya Watoto Katika Kukuza Maadili ya Jamii ya Wapemba.Tasinifu hii inalenga katika kuonesha mchango unaopatikana kupitia nyimbo za michezo ya watoto kwani kupitia nyimbo hizi jamii inapata kujifunza mengi tu kama vile, uvumilivu kwa wanandoa, uwajibikaji katika kazi, umuhimu wa usafi, nidhamu, umuhimu wa elimu na kadhalika. Hii inatokana na kwamba watu wengi walidhani kuwa hamuna mchango wowote unaopatikana kupitia nyimbo hizi. Mtafiti kwa kutumia nadharia ya uchambuzi matini, nadharia ya mwingiliano matini na mwitiko wa msomaji amefanikiwa kuonesha na kubainisha mchango hasa unaopatikana kupitia nyimbo za michezo ya watoto. Vile vile mtafiti alitumia mbinu ya kupitia machapisho mbali mbali na kwenda maskani Pandani, Uwondwe na Mzambarautakao katika wilaya ya Wete –Pemba kwa ajili ya kukusanya nyimbo, vyanzo vyake na maana zake. Nadharia hizo ndizo zilizomuongoza mtafiti katika uchanganuzi wa data katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kuwa nyimbo hizi asili yake haikuwa na lengo la kuburudusha tu kama ilivyokuwa mawazo ya wengi, lakini zilikuwa na lengo zaidi ya hilo kama vile kuelimisha, kuadilisha na kadhalika. Baada ya kuhakiki sampuli ya nyimbo imebainika kuwa nyimbo hizi husawiri maisha ya kinamama, baba na watoto wenyewe ambao mara nyingi ndio waimbaji wa nyimbo hizi katika michezo yao mbali mbali. Ingawa utafiti huu umeegemea upande wa ujumbe zaidi na jinsi fani inavyoibua ujumbe huo lakini bado kuna maeneo mengine ambayo yanahitaji kufanyiwa utafiti kupitia nyimbo hizi. Maeneo wenyewe ni kama vile ni jinsi gani sayansi na teknolojia (ugeni) unavyoadhiri nyimbo za michezo ya watoto na pia kuangalia muundo wa nyimbo hizo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 04 Mar 2020 12:55
Last Modified: 04 Mar 2020 12:55
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2469

Actions (login required)

View Item View Item