Masasa, Joseph Ismail
(2017)
Kuchunguza Athari ya Lugha ya Kijita katika Kujifunza Lugha ya Kiswahili.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu ni kujua jinsi ambavyo mtoto wa kijita anayejifunza lugha ya kiswahili anavyoathiriwa na lugha yake mama katika harakati zake za kujifunza lugha ya kiswahili sanifu. Utafiti huu umefanywa katika Wilayani Butiama.Taasisi mbili zilishilikishwa Shule ya Msingi Chimati A na Shule ya Msingi Bulinga A. Pia wataalamu (Wazazi) wa Vijiji hivyo Chimati na Bugunda. Utafiti huu umetumia mbinu ya dodoso, hojaji na mahojiano ya makundi katika kusanya data zake. Matokeo ya utafiti huu umebaini kwamba pana Athari ya Lugha ya Kijita katika kujifunza Lugha ya Kiswahili Sanifu. Hii inatokana na sababu ya Watoto kuhamisha uelewa wa Lugha ya Kwanza ya Kijita kwenda Lugha ya Pili ambayo ni lugha ya Kiswahili. Watoto walio wengi wana Athari ya Lugha Mama. Mapendekezo ya Mtafiti ni kwamba lugha ya kijita inaleta athari kwa watoto wa kijita na wajita wenyewe wanapokuwa wanajifunza lugha ya kiswahili sanifu. Hivyo pana haja ya kuanza kujifunza lugha hii ya Kiswahili katika mazingira ya nyumbani. Ili awe na uwezo wa kumdu kutumia kiswahili sanifu. Mtoto wa kijita akijifunza lugha ya kiswahili tangu utotoni kutamwezesha kuimudu lugha hii ya kiswahili sanifu, na hivyo kumsaidia kumdu somo lakiswahili shuleni pamoja na masomo mengine bila ya kuwa na usumbufu katika maendeleo yake kitaaluma ikizingatiwa kwamba takribani karibu shule zote za msingi za serikali nchini wanafunzi hufundishwa kwa kutumia lugha hii ya kiswahili sanifu isipokuwa somo la kiingereza. Hivyo kwa mtoto wa kijita kuimudu lugha hii ya kiswahili sanifu tangu utotoni ni hatua mojawapo muhimu katika maendeleo yake shuleni.
Actions (login required)
|
View Item |