Ulinganishi na Tofauti za Kifonolojia Kati ya Lahaja ya Kimakunduchi na Kitumbatu

Salum,, Hafsa Makame (2018) Ulinganishi na Tofauti za Kifonolojia Kati ya Lahaja ya Kimakunduchi na Kitumbatu. Masters thesis, The open University of Tanzania.

[thumbnail of HAFSA MAKAME SALUM.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (954kB) | Preview

Abstract

Tasnifu hii inachunguza ulinganifu wa kifonolojia kati ya lahaja ya Kitumbatu na lahaja ya Kimakunduchi. Utafiti uliofanywa uliongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni: kwanza, Kuchambua mlingano wa matamshi ya fonimu uliopo kati ya lahaja ya Kimakunduchi na lahaja ya Kitumbatu. Pili, Kuchambua tofauti za matamshi ya fonimu zilizopo kati ya lahaja ya Kitumbatu na Kimakunduchi. Na tatu ni Kuelezea mambo yaliyosababisha kulingana na kutofautiana kwa matamshi ya fonimu za lahaja ya Kitumbatu na Kimakunduchi. Mbinu zilizotumika katika ukusanyaji wa data niusaili na mahojiano. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu wakati wa ukusanyaji na uchambuzi wa data ni nadharia ya Isimu Linganishi na Konsonanti Vokali. Matokeo ya jumla ya utafiti huu yalionesha kuwa kuna mlingano na tofauti za kimatamshi katika fonimu za lahaja ya Kimakunduchi na Kitumbatu kama zifuatazo: kwa lahaja hizi zimelingana katika vipengele vifuatavyo; kuwa na silabi zenye sifa ya kudondosha fonimu, usilimisho wa matamshi ya fonimu na kuimarisha na kudhofisha matamshi ya fonimu. Pia, Lahaja hizi zimetofautiana katika vipengele vifuatavyo; ukakaishaji wa matamshi ya fonimu, lahaja moja kudhofisha na nyingine kuimarisha matamshi ya fonimu, uyeyushaji wa fonimu kwa lahaja pamoja na tofauti nyingine.Utafiti umebaini kuwa, ulinganifu na utofauti huo unatokana na kuwa ni lahaja zenye asili moja, kuwepo katika kundi moja la lahaja na wanajamii wake kuwa na nyanja za aina moja kiuchumi. Kutokana na matokeo haya, utafiti huu unapendekeza mambo yafuatayo: kwanza ni kutafiti juu ya athari za sayansi na teknolojia katika lahaja za Kiswahili. Pili, kutafiti juu ya mabadiliko ya kifonolojia katika lahaja za kiswahili,kwa kulinganisha miaka ya zamani na hali ya sasa ya lahaja hizo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 29 Feb 2020 10:16
Last Modified: 29 Feb 2020 10:16
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2437

Actions (login required)

View Item View Item