Kuchunguza Dhamira ya Mapenzi na Fani Katika Kitabu cha Mapenzi Bora cha Shaaban Robert

Zahor,, Fatmah Twalib (2017) Kuchunguza Dhamira ya Mapenzi na Fani Katika Kitabu cha Mapenzi Bora cha Shaaban Robert. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of FATMA TWALIB ZAHOR - TASINIFU-28-01-2017.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (425kB) | Preview

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza dhamira ya mapenzi na fani katika kitabu cha Mapenzi Bora cha Shaaban Robert. Ili kutimiza lengo kuu, kulikuwa na malengo mahsusi matatu; Kuainisha dhamira za mapenzi katika kitabu cha Mapenzi Bora, kuchambua dhamira za mapenzi zilizojitokeza katika kitabu cha Mapenzi Bora kuchunguza vipengele vya fani katika kitabu cha Mapenzi Bora. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini na mbinu ya maktabani. Data hizo zilikusanywa na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Matokeo ya kiutafiti yanaonesha kuwa katika kitabu cha mashairi cha Mapenzi Bora mtafiti ameainisha dhamira ya mapenzi katika makundi saba ambayo ni mapenzi ya Kimungu Mungu, mapenzi ya mitume, mapenzi ya sisi kwa sisi, mapenzi ya yasiyoangalia kabila, taifa wala rangi, mapenzi ya kupenda majirani na marafiki, mapenzi ya kudumu na mapenzi ya kupenda nchi. Dhamira hiyo ya mapenzi katika mafungu hayo saba, zinasisitiza mapenzi yaliyo ya ukweli ambayo yatasababisha kuwepo kwa amani na upendo miongoni mwa watu. Mapenzi ya kusaidiana katika shida na raha. Mapenzi ya kuvumiliana na kufanyiana subira katika matatizo, mapenzi ya kutokubaguana kwa kuangalia kabila, cheo, dini wala uzuri wa mtu, hayo ndiyo mapenzi ya kweli. Kwa upande wa fani vilivyoangaliwa ni vipengele vya lugha na muundo. Kuna tamathali za usemi nyingi ambazo ni takriri, tashibiha, tashihisi, sitiari, kejeli na taswira, pia kwa upande wa muundo ni tarbia, mizani nane, urari wa vina na mizani na kituo bahari.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 29 Feb 2020 09:52
Last Modified: 29 Feb 2020 09:52
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2432

Actions (login required)

View Item View Item