Kuchunguza Sanaa na Dhima za Methali za Wahaya

Kyabalishanga, Farida Hassan (2018) Kuchunguza Sanaa na Dhima za Methali za Wahaya. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU FARIDA-25-01-2018-Final.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (1MB) | Preview

Abstract

Mada ya utafiti huu ni Kuchunguza Sanaa na dhima za Methali za Wahaya. Ili kufanikisha mada hii mtafiti alikuwa na malengo mawili mahususi yafuatayo : kuchunguza sanaa inayopatikana katika methali za Wahaya na dhima inayopatikana katika methali za Wahaya. Malengo haya mawili yalifanyiwa kazi na matokeo ya utafiti yamepatikana kwa kutumia mbinu za majadiliano ya vikundi, usaili, lugha ya mazungumzo, utalii wa machapisho kutafuta data za upili na data za msingi ambazo zimekusanywa kutoka masikanini. Data zimechambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya Simiotiki na Sosholojia. Mtafiti alikusanya Methali 385. Zilizochambuliwa ni methali 179 ambazo zimepangwa katika makundi mawili. Makundi hayo ni Tamathali za semi pamoja na matumizi ya Taswira na Dhima. Katika tamathali za semi ni methali ishirini na nne (24), za lugha ya mafumbo, muundo katika methali, vina na mizani, takriri, tashibiha, tashihisi, sitiari, kejeli, tasifida, methali zinazokinzana na zinazorudia neno moja lakini mnyumbuliko tofauti. Matumizi ya Taswira ni methali ishirini na mbili (22) kama, taswira za wanyama, mazimwi, ndege, wadudu, makazi, silaha, viungo vya mwili pamoja na mazao/matunda. Na katika dhima ni methali mia moja thelathini na tatu (133), kama kuelimisha jamii methali, kukuza lugha, kukosoa jamii, mila na desturi, kupatanisha, malezi ya watoto, kuhimiza undugu, kuthamini chako, tahadhali/onyo, umoja na juhudi, faraja/ kutiana moyo na zinazowahusu wanaume na wanawake, kuburudisha. Ambazo hazijachambuliwa ni methali 206. Kwa kuzingatia umuhimu wa methali katika jamii ya Wahaya, mtafiti aliona naye aweke juhudi zake katika kuchunguza sanaa na dhima za methali za Wahaya.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 14 Oct 2018 11:04
Last Modified: 14 Oct 2018 11:04
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2272

Actions (login required)

View Item View Item