Kutathmini Matumizi ya Lugha na Dhamira Katika Tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani: Utafiti Linganishi

Fides, Cyprian (2017) Kutathmini Matumizi ya Lugha na Dhamira Katika Tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani: Utafiti Linganishi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU  - CYPRIAN FIDES, FINAL.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (836kB) | Preview

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu ni kutathmini matumizi ya lugha na dhamira zilizojitokeza katika tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani: Utafiti linganishi. Ili kufanikisha utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu za maktabani katika kukusanya na kuwasiilisha data kimaelezo. Pia marejeleo mbalimbali kutoka tamthiliya za Kiswahili yalipitiwa. Nadharia ya fasihi ya jamii ndiyo iliyotumika katika kufanikisha utafiti huu. Nadharia hii imemsaidia mtafiti kuweza kubaini mawazo mbalimbali ya waandishi katika tamthiliya zao za utafiti linganishi. Matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti. Tamthiliya hizi teule zimebainisha jamii yetu kabla ya uhuru na baada ya uhuru. Dhamira za uongozi mbaya, rushwa na usaliti zimejitokeza. Matokeo mengine ni dhamira ya ukombozi iliyomfanya mkoloni aondolewe katika ardhi ya jamii ya watu wa Kusini ili wawe huru, kutumia ardhi yao na mali nyingine zilizopatikana katika jamii yao. Pia uzalendo ulitakiwa kwa jamii kwa kuwapeleka vijana kwenye mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa na tohara. Tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani zina mchango mkubwa katika jamii kwa kuwasilisha ujumbe ambao ni wa kihistoria unaoiwezesha kujua matukio mbalimbali ya nchi kabla na baada ya uhuru

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 14 Oct 2018 11:01
Last Modified: 14 Oct 2018 11:01
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2271

Actions (login required)

View Item View Item