Juma, Mohammed Soud
(2017)
Kuchunguza Matumizi ya Lugha Katika Riwaya ya Kichwamaji na Vuta N’kuvute : Utafiti Linganishi.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu unahusu Kuchunguza Matumizi ya Lugha Katika Riwaya ya Kichwamaji na Vuta n’kuvute – Utafiti linganishi. Tasinifu hii imekusudia katika kuonesha matumizi ya lugha kwenye kipengele cha tamathali za semi zilizotumika katika riwaya teule. Pia kuonesha namna waandishi hawa walivyofana na kutofautiana katika matumizi ya tamathali ya semi na namna zilivyoibua dhamira mbalimbali. Utafiti huu umeongozwa na nadharia kuu mbili. Nazo ni nadharia ya simiotiki ambapo imemwezesha mtafiti kubaini tamathali za semi mbalimbali. Na nadharia ya udhanaishi iliyoweza kuibua dhamira mbalimbali kutoka katika riwaya hizo teule. Kwa upande wa mbinu za kukusanyia data, mtafiti alitumia mbinu ya kimaktaba kwa kuanza kuvidurusu vitabu teule na kuyaelewa kwa undani maudhui yaliyokusudiwa na waandishi wa vitabu hivyo. Kisha mtafiti akarudia kuvisoma kwa umakini zaidi kwa kudondoa kila tamathali ya semi aliyoikuta na kuitayarishia jedwali lake maalumu. Baadae mtafiti akutoa dhamira zilizojitokeza kutoka katika tamathali za semi. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa waandishi wote wawili wamefanana kwa kutumia tamathali za semi kumi na moja (11). Na mwishowe tamathali za semi hizo zimeweza kutoa dhamira ishirini na mbili (22). Na kubainika kuwa wamefanana katika tamathali za semi na wametofautiana kwa upande wa dhamira na hili limetokana na kuwa riwaya ya Kichwamaji ni fupi kidogo kulinganisha na riwaya ya Vuta n’kuvute.
Actions (login required)
|
View Item |