Kuchunguza Fasihi ya Majina ya Mitaa Mjini Unguja

Hassan, Halima Ali (2017) Kuchunguza Fasihi ya Majina ya Mitaa Mjini Unguja. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU - HALIMA ALI HASSAN.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (316kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulichunguza fasihi ya majina ya mitaa ya Mjini Unguja. Ndani ya majina ya mitaa mna siri nyingi zilizojificha zinazohitaji uweledi ili kuweza kuzifumbua. Mtafiti amechunguza fasihi ya majina ya mitaa kwa kubainisha fani iliyounda majina hayo kwa kuchambua kipengele cha mtindo na lugha ya kifasihi iliyotumika. Vilevile, alichambua maudhui kwa kubainisha asili ya majina ya mitaa na ujumbe, kwa kuongozwa na nadharia ya uhalisia na nadharia ya ndani nje. Utafiti umefanyika katika maeneo ya Mjini Unguja ndiko watafitiwa walikosailiwa. Jambo la kufurahisha na la kutia moyo ni ushiriki wa viongozi wa juu wa Serikali na wazee mashuhuri, katika kutoa data zilizofanikisha utafiti huu. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa majina ya mitaa yanachambulika kifasihi. Kwa Ujumla, utafiti uliongozwa na madhumuni matatu ambayo yalisaidia kubainisha fasihi ya majina ya mitaa iliyopo Mjini Unguja. Madhumuni ya kwanza kuchambua asili ya majina ya mitaa matokeo yameonesha kuwa majina hayo yameanza kwa sababu maalumu ya kihistoria na kimazingira. Madhumuni ya pili kuchunguza vipengele vya fani ambavyo ni lugha na mtindo. Matokeo yanaonesha kuwa, majina ya mitaa yameundwa kutokana na kaida maalum kama vile, mbinu ya umashuhuri, mbinu ya mazingira na usababishi. Majina ya mitaa yameundwa kwa kutumia lugha ya kifasihi yenye mvuto, inayotoa taswira kwa jamii yenye tamathali za semi kama vile tashbiha, tauria, tash hisi, mafumbo na tanakali sauti. Madhumuni ya tatu kueleza ujumbe unaopatikana katika majina ya mitaa Mjini Unguja. Matokeo yameonesha kuwa majina yanatoa ujumbe wa jumla kama vile kulinda utamaduni, utambulishi na kuhifadhi historia.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 09 Oct 2018 07:29
Last Modified: 09 Oct 2018 07:29
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2203

Actions (login required)

View Item View Item