Kuchunguza Dhamira za Nyimbo Bembelezi za Watoto Katika Lahaja ya Kimakunduchi

Haji, Zainab Ramadhan (2017) Kuchunguza Dhamira za Nyimbo Bembelezi za Watoto Katika Lahaja ya Kimakunduchi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ZAINAB RAMADHAN HAJI-TASNIFU-13-10-2016.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (536kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu umeshughulikia dhamira katika nyimbo bembelezi za watoto mifano kutoka Makunduchi. Ili kukamilisha lengo hili kuu, malengo mahsusi mawili yamepitiwa. Malengo hayo yalihusu kuchambua dhamira na mbinu za kisanaa zinazotumiwa na wasanii katika kusawiri dhamira zinazojitokeza ndani ya nyimbo za kubembelezea watoto mifano kutoka Makunduchi. Katika kukusanya data mtafiti alitumia mbinu ya kupitia machapisho, mbinu ya ushuhudiaji, mbinu ya kusikiliza na mbinu ya mahojiano pamoja na kutumia mbinu ya kimaelezo katika kuchambua data. Kwa ujumla utafiti umeweza kukusanya data ambazo zimeweza kujibu maswali ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba, nyimbo bembelezi za watoto zina hazina kubwa katika kuonyesha dhamira ambazo zinakwenda sambamba na uhalisia katika maisha na jamii. Dhamira hizo ni kama mapenzi, nafasi ya mwanamke, ukweli, usaliti, siasa na uchumi. Pia, matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba mbinu za kisanaa zinazotumiwa na watunzi pamoja na wasanii katika uwasilishaji wa dhamira ni nyingi miongoni mwake ni kama taswira, ishara, sitiari, usimulizi, usambamba, nahau, tashbiha na takriri. Mwishoni mwa utafiti kumetolewa mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya tafiti za baadaye kwa kupitia utanzu wa fasihi simulizi wa nyimbo kwa kuziangalia zaidi nyimbo bembelezi za watoto mifano kutoka sehemu nyengine zinazopatikana ndani ya nchi na katika lugha za makabila mengine nchini.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 Oct 2018 18:02
Last Modified: 05 Oct 2018 18:02
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2135

Actions (login required)

View Item View Item