Haji, Zainab Ramadhan
(2017)
Kuchunguza Dhamira za Nyimbo Bembelezi za Watoto Katika Lahaja ya Kimakunduchi.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia dhamira katika nyimbo bembelezi za watoto mifano kutoka Makunduchi. Ili kukamilisha lengo hili kuu, malengo mahsusi mawili yamepitiwa. Malengo hayo yalihusu kuchambua dhamira na mbinu za kisanaa zinazotumiwa na wasanii katika kusawiri dhamira zinazojitokeza ndani ya nyimbo za kubembelezea watoto mifano kutoka Makunduchi. Katika kukusanya data mtafiti alitumia mbinu ya kupitia machapisho, mbinu ya ushuhudiaji, mbinu ya kusikiliza na mbinu ya mahojiano pamoja na kutumia mbinu ya kimaelezo katika kuchambua data.
Kwa ujumla utafiti umeweza kukusanya data ambazo zimeweza kujibu maswali ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba, nyimbo bembelezi za watoto zina hazina kubwa katika kuonyesha dhamira ambazo zinakwenda sambamba na uhalisia katika maisha na jamii. Dhamira hizo ni kama mapenzi, nafasi ya mwanamke, ukweli, usaliti, siasa na uchumi. Pia, matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba mbinu za kisanaa zinazotumiwa na watunzi pamoja na wasanii katika uwasilishaji wa dhamira ni nyingi miongoni mwake ni kama taswira, ishara, sitiari, usimulizi, usambamba, nahau, tashbiha na takriri. Mwishoni mwa utafiti kumetolewa mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya tafiti za baadaye kwa kupitia utanzu wa fasihi simulizi wa nyimbo kwa kuziangalia zaidi nyimbo bembelezi za watoto mifano kutoka sehemu nyengine zinazopatikana ndani ya nchi na katika lugha za makabila mengine nchini.
Actions (login required)
|
View Item |