Changamoto za Kutafsiri Riwaya: Mifano Kutoka Tafsiri ya Kiswahili ya Riwaya ya Robinson Crusoe

Fakih, Ali Hemed (2018) Changamoto za Kutafsiri Riwaya: Mifano Kutoka Tafsiri ya Kiswahili ya Riwaya ya Robinson Crusoe. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU-TAFSIRI (ALI)  MUDHAMIRI - FINAL.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (1MB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu changamoto za kutafsiri riwaya kutoka katika lugha ya Kiingereza kwenda katika lugha ya Kiswahili kwa kutumia mfano wa riwaya ya Robinson Crusoe. Lengo la utafiti huu ni kuchuguza changamoto za kutafsiri riwaya kutoka katika lugha ya Kiingereza kwenda katika lugha ya Kiswahili kwa kutumia mfano wa riwaya ya Robinson Crusoe iliyotafiriwa kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili ili kubaini matatizo na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na nazo. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi wa madhumuni maalum, wakati ambapo data zilikusanywa kwa kutumia mbinu tatu, ambazo ni mapitio ya maandiko, usaili na hojaji. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa kutumia mbinu ya uchambuzi maudhui. Aidha Skopos ilitumika kukusanya, kuchambua na kujadili data za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa, changamoto za kutafsiri riwaya ni pamoja na changamoto za kiisimu, kiutamaduni na uteuzi mbaya wa visawe. Aidha, utafiti huu ulibaini kuwa miongoni mwa sababu zinazosababisha changamoto hizo ni pamoja na tofauti za lugha na tofauti za kiutamaduni baina ya lugha chanzi na lugha lengwa.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 Oct 2018 17:40
Last Modified: 05 Oct 2018 17:40
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2128

Actions (login required)

View Item View Item