Tathmini ya Maanana Vigezo Vilivyotumika Kutoa Majina ya Utani kwa Jamii ya Wapemba

Masoud, Rashid Sinani (2018) Tathmini ya Maanana Vigezo Vilivyotumika Kutoa Majina ya Utani kwa Jamii ya Wapemba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASNIFU - Masoud final - HABIBA.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (1MB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulihusu tathmini ya maana na vigezo vilivyotumika kutoa majina ya utani: Kwa mfano kutoka jamii ya Wapemba. Utafiti huu uliongozwa na malengo mawili mahsusi ambayo ni: Kutathmini maana ya majina ya utani ya Kiswahili kwa jamii ya Wapemba na kuainisha vigezo vinavyotumika kupata majina ya utani ya jamii ya Wapemba. Utafiti ulifanyika Mkoa wa Kaskazini Pemba. Utafiti umekusanya data za uwandani kwa kutumia mbinu za hojaji na mahojiano. Watafitiwa walikuwa 428 na usamplishaji nasibu ulitumika kupata data za utafiti. Nadharia mbili zilitumika; i. Uchanganuzi Hakiki na Usemi wenye msingi wa kutambua uamilifu wa lugha katika jamii unaokitwa katika muktadha wa matumizi na ii. Nadharia ya Maana ya Umaanishaji ambayo msingi wake ni kutoa tafsiri ya maana kimuktadha pamoja na elimu shirikishi baina ya msikilizaji na msemaji. Utafiti umebaini kuwa majina ya utani hayatolewi kiholela bali kuna vishawishi vinavyochochea uibukaji wa majina hayo ambavyo huakisi masuala mbalimbali ya kijamii kama vile; matukio ya kihistoria, shughuli za mhusika binafsi, urithi kutoka kwa wazazi, umbile la mhusika na visa au matukio aliyoyafanya mhusika. Matokeo ya utafiti huu yamethibitisha kuwa majina ya utani hufungamana na jamii husika. Picha halisi ya maana zinazopatikana katika majina ya utani, yanaonekana kubeba uhalisia wa mhusika kwa tabia, sifa, historia na hata eneo analoishi au asili ya mhusika. Utafiti umebaini kuwa maeneo ambayo majina ya utani yanatumiwa yameonekana kumjengea mhusika umaarufu zaidi ukilinganisha na majina halisi. Kwa vile utafiti huu umetathmini maana na vigezo vilivyotumika kupata majina ya utani kutoka jamii ya Wapemba, tafiti zaidi zinahitajika kuchunguza athari na umuhimu wa majina ya utani kwa jamii hiyo au jamii nyenginezo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 Oct 2018 17:26
Last Modified: 05 Oct 2018 17:26
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2123

Actions (login required)

View Item View Item