Kuchunguza Taswira ya Mwanamke katika Ngano za Jamii ya Wanyamwezi

Mwakila, Neema Uswege (2017) Kuchunguza Taswira ya Mwanamke katika Ngano za Jamii ya Wanyamwezi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA MWAKILA-26-01-2017.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (545kB) | Preview

Abstract

Mada ya utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza Taswira ya mwanamke katika Ngano za Jamii ya Wanyamwezi. Lengo kuu la utafiti lilifungamana na mada ya utafiti huku malengo ya utafiti yakiwa ni kuchambua taswira ya mwanamke katika ngano za Wanyamwezi na kuelezea uhalisia wa taswira ya mwanamke katika ngano za Wanyamwezi kwa jamii ya leo. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za usaili na upitiaji wa nyaraka na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia ya Ufeministi. Matokeo ya utafiti yanabainisha kuwa ngano za jamii ya Wanyamwezi zinamsawiri mwanamke kwa namna mbalimbali. Mwanamke anasawiriwa kama kiumbe katili, mwanamke ni kiumbe asiyependa watoto wa kambo, mwenye nguvu na akili nyingi, kutoshirikishwa katika maamuzi, mtu mwenye huruma, mtu mwenye busara na hekima na kiumbe mwema. Taswira hii ya mwanamke inayojitokeza katika ngano za jamii ya Wanayamwezi zina uhalisia katika maisha ya leo kwani wapo wanawake ambao wana tabia na mwenendo wa aina hii. Wapo wanawake wema na wapo wengine ambao ni waovu.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 Oct 2018 17:20
Last Modified: 05 Oct 2018 17:20
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2121

Actions (login required)

View Item View Item