Asili ya Majina ya Mahali na Dhima zake katika Jamii Kisiwani Pemba

Mohamed, Sharifa Rashid (2018) Asili ya Majina ya Mahali na Dhima zake katika Jamii Kisiwani Pemba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Sharifa Rashidi Mohamed.docx] PDF - Submitted Version
Download (125kB)

Abstract

Utafiti huu umeshughulikia asili ya majina ya mahali na dhima zake katika jamii kisiwani Pemba. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza asili ya majina ya mahali na dhima zake katika jamii kisiwani Pemba. Utafiti huu ulifanyika katika Wilaya ya Wete na Chake Chake. Utafiti huu umetumia mkabala wa kimaelezo na sampuli iliyotumika ni sampuli ya kukusudia na sampuli bahatishi. Mbinu zilizotumika kukusanya data ni hojaji pamoja na dodoso. Matokeo ya utafiti huu ni kuwa asili ya majina ya mahali kisiwani Pemba hutokana na sababu za kijiografia, vyanzo vya maji, hali ya kiuchumi, umbali wa maeneo,imani,itikadi na hata kazi na tabia za watu. Pia huwa na miundo tofauti kama vile uradidi,ufupishaji,muambatano,utohoaji,unyambuaji na miundo menginevyo. Majina hayo hubeba dhima nyingi kama vile huruma na kusaidiana,mahusiano ya kimapenzi,shughuli za kijamii na dhima nyingi nyenginezo. Mapendekezo yanayotokana na utafiti huu ni kuwa kufanyike tafiti zitakazozingatia maumbo na michakato inayotumika kuunda majina ya mahali kisiwani Pemba.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 Oct 2018 16:44
Last Modified: 05 Oct 2018 16:44
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2111

Actions (login required)

View Item View Item