Uchunguzi wa Ukahaba katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano katika Vuta N’kuvute na Tata za Asumini.

Khamis, Saumu Juma (2017) Uchunguzi wa Ukahaba katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano katika Vuta N’kuvute na Tata za Asumini. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of SAUMU JUMA KHAMIS.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (658kB) | Preview

Abstract

Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza suala la Ukahaba katika riwaya ya Kiswahili kwa kutumia mifano kutoka katika riwaya ya Vuta N’kuvute na Tata za Asumini. Pia, malengo mahususi ya Tasnifu hii ni matatu; ambayo ni kubainisha usawiri wa Ukahaba na wahusika makahaba katika riwaya za Vuta N’kuvute na Tata za Asumini, kulinganisha sababu za Ukahaba zinazojitokeza katika riwaya hizo na uhalisia wake katika jamii na kuonyesha athari za Ukahaba kwa wahusika na jamii kwa ujumla. Data za utafiti huu zimekusanywa kutoka maktabani na uwandani ambapo data za maktabani zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji maandiko na data za uwandani zimekusanywa kwa kutumia mbinu tatu za ukusanyaji data. Mbinu hizo ni majadiliano ya vikundi, usaili na hojaji. Nadharia ya Uhalisia na Nadharia ya Saikochanganuzi zimetumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za utafiti huu. Utafiti huu umebaini kuwa riwaya za Kiswahili zinatumia baadhi ya wahusika kusawiri suala la Ukahaba. Usawiri huu unadhihirisha uhalisia uliomo katika jamii na jinsi riwaya za Kiswahili zinavyowasilisha suala la Ukahaba na mtazamo wa jamii kuhusu Ukahaba. Aidha, utafiti umebaini sababu kadhaa za Ukahaba zilizojibainisha kutoka kwenye riwaya teule na zilizowasilishwa na wanajamii. Sababu hizo ni pamoja na umasikini, starehe, mazoea, kwenda na wakati, na ukosefu wa malezi. Pia, utafiti umegundua kwamba Ukahaba una athari kwa wahusika na jamii kwa ujumla. Zaidi ya hayo, utafiti huu umebaini kuwa waandishi kwa kiasi kikubwa wanawatumia wahusika wa kike tu kuwasawiri kama makahaba japokuwa kwa kiasi fulani wasanii hao wameshindwa kuwahusisha wahusika wa kiume moja kwa moja kama makahaba.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 Oct 2018 16:33
Last Modified: 05 Oct 2018 16:33
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2108

Actions (login required)

View Item View Item