Kutathmini Matumizi ya Mtindo na Dhamira katika Tamthiliya za Mashetani na Mashetani Wamerudi: Utafiti Linganishi

Massoud, Safia Said (2018) Kutathmini Matumizi ya Mtindo na Dhamira katika Tamthiliya za Mashetani na Mashetani Wamerudi: Utafiti Linganishi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of SAFIA  SAID MASSOUD TASNIFU.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (672kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu Kutathmini matumizi ya Mitindo na Dhamira katika Tamthiliya ya Mashetani na Mashetani Wamerudi. Utafiti huu ni wa maktabani ambao ulitumia sampuli lengwa nakuongozwa na Nadharia yaMuingilianomatini na Nadharia yaFasihi linganishi.Utafiti uligundua kuwa tamthiliya ya Mashetani imetumia vipengele vya kimtindo vinavyohusiana na matumizi ya lugha kama vile uteuzi wa msamiati pamoja na matumizi ya tamathali za semi. Mbinu nyenigine za kimtindo zilizotumika katikaTamthiliya za Mashetani na Mashetani Wamerudi mbinu hizo ni kama vile mandhari za fasihi simulizi, mtindo wa nyimbo, masimulizi, matumizi ya nafsi zote,majigambo, dayalojia na mtindo wa tamthiliya za majaribio. Piatamthiliya zote zimelingana kwa kutumia mtindo wa mashairi, nyimbo, majigambo, matumizi ya nafsi, mandhari ya fasihi simulizi, wahusika wa fasihi simulizi, matumizi ya ndoto,tamthiliya ya majaribio na mtindo wa masimulizi. Vile vile, zimelingana katika kutumia methali, nahau, misemo, jazanda, ishara, taswira na tamathali za semiImegundulikakuwa kuna tofauti ndogo kati ya tamthiliya teule ambapoMashetani imetumia mchezo ndani ya mchezo ambapo mtindo huu hauko katika Mashetani Wamerudi. Taswira kama vile punda, jogoo, simba, batamzinga, kuku hazijitokezi katika tamthiliya ya Mashetani.Aidha, utafiti umegundua kuwa kuna kufanana kwa dhamira katika Tamthiliya teule. Tamthiliya hizi zimejadili dhamira za ukoloni mamboleo, harakati za ukombozi, ujenzi wa jamii mpya, nafasi ya mwanamke, matabaka, uongozi mbaya na ubadhirifu wa mali za umma, ukosefu wa demokrasia na elimu ya Kimagharibi. Pia, kunadhamira ya utandawazi, kujitoa mhanga, umoja na mshikamano, athari za utandawazi na ukosefu wa ajira hazijitokezi katika Tamthiliya ya Mashetani.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 Oct 2018 16:23
Last Modified: 05 Oct 2018 16:23
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2105

Actions (login required)

View Item View Item