Kuchunguza Ubiblia Katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo

Msangi, Emmanuel Oscar (2018) Kuchunguza Ubiblia Katika Tamthiliya za Emmanuel Mbogo. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of MSANGI, Emmanuel-Dissertation.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (673kB) | Preview

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kuchunguza ubiblia katika tamthiliya za Emmanuel Mbogo kupitia tamthiliya zake za Nyerere na Safari ya Kanaani (2015) na Sadaka ya John Okello (2015). Ili kufikia lengo kuu tulikuwa na malengo mahsusi mawili; kubainisha utokezaji wa Ubiblia katika tamthiliya za Emmanuel Mbogo na kueleza sababu za utokezaji wa Biblia/mwangwi wa Biblia katika kazi hizo teule za Emmanuel Mbogo. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji lengwa. Tamthiliya teule za Sadaka ya John Okello na Nyerere na Safari ya Kanaani, ziliteulewa kwa maksudi kabisa kwa kuwa ndizo ambazo zimeweza kumpatia mtafiti data alizozihitaji. Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makini. Uchambuzi wa data katika utafiti huu ulifanywa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo. Aidha ukusanyaji, uchambuzi na kujadili data kuliongozwa na nadharia ya mwingilianomatini. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa kuna Ubiblia mwingi katika tamthiliya za Emmanuel Mbogo alizoziandika miaka ya karibuni. Vipengele vya kifani ndivyo vimetumika katika kubainisha ubiblia huo. Vipengele hivyo ni jina la kitabu, hadithi za kibiblia, wahusika wa kibiblia, nukuu za kibiblia na mtindo wa ushairi. Tamthiliya hizi mbili tulizozitafiti za Emmanuel Mbogo; Sadaka ya John Okello na Nyerere na Safari ya Kanaani zimeakisi mwangwi mkubwa wa Biblia. Kwa mfano kisakale cha wana wa Israel kukaa utumwani Misri na kisha kuanza safari kurejea kwao Kanaani katika Biblia kinapatikana kitabu cha “Kutoka”. Kisakale hiki kimeakisiwa kwa wingi katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani, Kanaani ni nchi iliyojaa maziwa na asali kwa mujibu wa kisakale hicho.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 05 Oct 2018 15:29
Last Modified: 05 Oct 2018 15:29
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2091

Actions (login required)

View Item View Item