Kutathmini Usawiri wa Mwanamke Katika Riwaya ya Mfadhili

Masoud, Hemed Said (2018) Kutathmini Usawiri wa Mwanamke Katika Riwaya ya Mfadhili. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of HEMED SAID MASOUD -IKISIRI-13-02-2018.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (819kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu, Kutathmini usawiri wa mwanamke katika riwaya ya Mfadhili. Kwa nia ya kufanikisha lengo kuu la utafiti huu ambalo ni Kutathmini usawiri wa mwanamke katika riwaya ya Mfadhili, utafiti uliambatanishwa na malengo mahususi mawili yafuatatyo: Mosi, Kubainisha taswira mbalimbali za mwanamke alivyochorwa katika riwaya ya Mfadhili. Pili, Kuelezea sababu zinazomfanya mwanamke huyo asawiriwe hivyo alivyosawiriwa katika riwaya teule ya Mfadhili. Utafiti huu umetumia mbinu ya maktabani kupitia usomaji makini na upitiaji wa nyaraka. Sambamba na hayo mkabala wa uchambuzi wa data uliotumika ni wa Kimaelezo kwa kiwango kikubwa na mkabala wa kitakwimu kwa kiwango kidogo. Katika kufikia malengo ya utafiti huu, mtafiti alitumia nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika kwa lengo la kumsawiri mwanamke kwa undani zaidi na kuweza kuelewa ni kwa jinsi gani msanii au mwandishi alivyotumia ufundi wake kumchora mwanamke katika hali chanya na hasi. Mtafiti ameweza kuyaona hayo kwa kupitia riwaya hiyo teule ya Mfadhili. Miongoni mwa usawiri huo mtafiti ameona mwanamke amesawiriwa kwa tabia / matendo chanya (mema) kama kiongozi bora, mshauri mwema, msamehevu, mwenye huruma, msuluhishaji, mwenye mapenzi ya dhati nk. Pia utafiti huu umebaini tabia hasi (mbaya) kwa mwanamke kama vile, ulevi, usaliti, kukosa msimamo, mwenye uchu wa madaraka nk. Pamoja na hayo mtafiti amebaini sababu za mwanamke kusawiriwa hivyo ni pamoja na kutekeza wajibu wake kazini, kujenga upendo na huruma. Bila shaka mtafiti hapa amekusudia kusema kwamba tabia nzuri ndizo za kufuatwa na tabia mbaya ndio za kuachwa na hiyo ndio siri ya mafanikio.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 04 Oct 2018 16:47
Last Modified: 04 Oct 2018 16:47
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2069

Actions (login required)

View Item View Item