Tofauti za Msamiati katika Muktadha Mbali Mbali wa Lahaja ya Kipemba na Kiswahili Sanifu

Ghaithuu, Salim Suleiman (2017) Tofauti za Msamiati katika Muktadha Mbali Mbali wa Lahaja ya Kipemba na Kiswahili Sanifu. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of GHAITHUU SALIM SULEIMAN FINAL VERSION.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (718kB) | Preview

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza tofauti za lahaja ya Kipemba katika lugha ya Kiswahili sanifu na jinsi athari hizo zinavyosababisha ama kuwepo au kutokuwepo mawasiliano fanisi baina ya wasemaji wa lugha ya Kiswahili. Ikiwa ni hatua moja wapo ya kuitafiti lugha ya Kiswahili na lahaja zake, ambapo tasnifu hii imeangalia watu wanaoishi mjini na vijijini. Mbinu ya dodoso, mahojiano, na ushuhudiaji ndizo zilizotumika katika kukusanyia data, ambapo Sampuli ya unasibu ndio iliyotumika katika kuchagua watoa taarifa kwani kila memba katika kundi lengwa ana haki ya kushiriki. Nadharia ya isimu fafanuzi imetumika kufafanua na kuchunguza kipengele cha tofauti za msamiati katika muktadha mbali mbali wa lahaja ya Kipemba na Kiswahili sanifu. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa jamii ya vijijini (Micheweni, Kojani, Wingwi) bado wanazungumza lahaja ya Kipemba lakini jamii (watu) wa mjini Wete wao hutumia Kiswahili Sanifu na kwa ufasaha. Pia kupitwa na wakati kwa mila, desturi, na tamaduni za jamii ya Kipemba na kulazimika kuiga tamaduni za kigeni mfano mavazi na mapambo ya harusi na ngoma. Ninapendekeza kuwa uchunguzi zaidi ufanyike kwa kuangalia asili ya lahaja ya kipemba na kuchunguza kipengele cha sintaksia (miundo ya sentensi) na mofolojia katika lahaja ya Kipemba. Vile vile utafiti huu ulihusu msamiati wa matukio ya harusi na msibani tu, iko haja ya utafiti zaidi ufanyike kuhusu matukio mengine kama vile shughuli za kilimo, biashara, usafiri na uchukuzi katika nchi kavubaharini, na hewani (usafiri wa ndege), dini, elimu katika skuli za msingi na za sekondari, mahakamani, utawala na mengine mengi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 04 Oct 2018 16:21
Last Modified: 04 Oct 2018 16:21
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2067

Actions (login required)

View Item View Item