Saleh, Mwajuma Ali
(2018)
Changamoto za Kutafsiri Sentensi za Kiswahili Sanifu Zenye Utata kwenda Kiingereza.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Utafiti huuulilenga kuchunguza changamoto zilizopo katika kutafsiri tungo tata za lugha ya Kiswahili kwenda lugha ya Kiingereza na madhara yake katika ufanisi wa mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji wa lugha hizo mbili. Utafiti huu umetumia mkabala wakimaelezo na kitakwimu katika kuchunguza, kuchambua na kujadili data na matokeo ya utafiti huu. Utafiti huu ulifanyika katika Mkoa wa Mjini Magharibi katika Wilaya ya Magharibi A na B na Wilaya ya Mjini. Mbinu zilizotumika kukusanya data za utafiti huu ni tatu yaani, usomaji wa machapisho, dodoso na usaili. Aidha, utafiti huu ulitumia sampuli nasibu kuteua walengwa wa utafiti. Watafitiwa 100, ikiwa ni pamoja na wanawake50 na wanaume 50 ndio waliotumika katika utafiti huu. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Ulinganifu wa kimuundokatika kukusanya, kuchambua na kujadili data na matokeo ya utafiti. Utafiti huu umebaini kuwa kuna tungo zenye utata katika Kiswahili. Aidha, utafiti huu umebaini kuwa kuna changamoto za kutafsiri tungo tata za Kiswahili kwenda katika Kiingereza. Miongoni mwa changamoto hizo ni kukosekana kwa visawe, changamoto ya kiutamaduni, Changamoto inayotokana na tofauti za kimaeneo (lahaja), changamoto za kiisimu, kimuktadha na changamoto inayotokana na miundo ya sentensi. Vile vile utafiti huu ulibaini kuwa changamoto hizo zina athari katika mawasiliano kwa sababu husababisha upotofu wa maana na ujumbe, kupotosha muundo wa tungo za matini chanzi, kukosekana kwa ushikamani wa ujumbe na kukosekana kwa ushikamani wa matini chanzi na matini lengwa. Utafiti huu unapendekza kwamba tafiti zingine zinaweza kufanyika ili kuchunguza changamoto za kutafsiri tungo tata za lugha zingine.
Actions (login required)
|
View Item |