Mlambia, Anna Michael
(2017)
Kuchunguza Dhima za Nyimbo za Asili za Watoto za Wahehe.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Mada ya utafiti huu ilikuwa ni Kuchunguza dhima za nyimbo za asili za watoto za Wahehe. Mada hii ya utafiti ilikuwa na malengo mahususi mawili ambayo yalikuwa ni kuchambua dhima za nyimbo za asili za watoto za Wahehe wa mkoani Iringa na kubainisha nafasi ya nyimbo za asili za watoto za Wahehe katika jamii hiyo. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu za ushuhudiaji, usaili na hojaji na kuchambuliwa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na nadharia za Uamilifu, Uasilia na Uhalisia. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa nyimbo za asili za watoto za Wahehe zina dhima muhimu katika jamii hiyo. Dhima hizo ni pamoja na Kuhamasisha maadili mema, kuonya jamii, kuelimisha jamii, kuchapulisha kazi, kutunza mila na desturi, Kupiga vita uchawi, kuagana na wazazi na kudumisha heshima katika jamii. Dhima hizi zina nafasi kubwa katika kuifanya jamii ya Wahehe kuwa yenye umoja na mshikamano katika maisha yao ya kila siku
Actions (login required)
|
View Item |