Kutathimini Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo na Asali Chungu: Utafiti Linganishi

Haji, Ali Vuai (2018) Kutathimini Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Dunia Uwanja wa Fujo na Asali Chungu: Utafiti Linganishi. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Ali Vuai Tasnifu.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (576kB) | Preview

Abstract

Lengo la utafiti huu ni Kutathimini Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Dunia uwanja wa fujo na Asali chungu: Utafiti Linganishi. Ili kukamilisha lengo hili,utafiti ulikuwa na malengo mahususi matatu ambayo ni; Kuainisha Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Dunia Uwanja wa fujo, Kuainisha Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika Riwaya ya Asali chungu na mwisho ni Kulinganisha na Kulinganua Mbinu za Usawiri wa Wahusika katika riwaya teule za Dunia Uwanja wa fujo na Asali Chungu.Data za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka maktabani. Mkabala wa kimaelezo sambamba na Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji na Fasihi Linganishi ndizo zilizotumika katika kuchambua data za utafiti. Mtafiti alitumia nadharia hii kwa lengo la kuwasawiri wahusika na alitumia nadharia ya Fasihi Linganishi kwa lengo la kulinganisha na kulinganua mbinu za usawiri wa wahusika katika riwaya hizi mbili. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa mbinu za usawiri wa wahusika ambazo mtafiti amezibaini ni pamoja na Mbinu ya Kimaelezi, mbinu ya Uzungumzi nafsi, mbinu ya kidrama, mbinu ya kuwatumia wahusika wengine, mbinu ya motifu ya safari, mbinu ya taharuki, na mbinu ya majazi au majina.Mtafiti alibaini kuwa riwaya hizi zimetafautiana sana katika kumsawiri mhusika kwani watunzi wa riwaya hizi wanatoka na wana asili ya jamii mbili tofauti na bila shaka hata mitazamo ya dini, hisia zao ni tofauti.Kwa mfano Said A.Mohamed ni mwandishi kutoka Zanzibar na ni muumini wa dini ya Kiislamu na Kezilahabi ni mwandishi kutoka Tanzania bara, Kisiwa cha Ukerewe na ni muumini wa dini ya Kikristo.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 01 Oct 2018 14:28
Last Modified: 01 Oct 2018 14:28
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2013

Actions (login required)

View Item View Item