Tathmini ya matumizi ya Semi katika Mabango ya Biashara: Mifano kutoka Pemba

Ali, Abdulla Haji (2017) Tathmini ya matumizi ya Semi katika Mabango ya Biashara: Mifano kutoka Pemba. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of A H A TATHMINI.doc] PDF - Submitted Version
Download (20MB)

Abstract

Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa ni kutathimini matumizi ya semi katika mabango ya biashara. Ili kufikia lengo kuu utafiti huu uliongozwa na malengo mahususi matatu mosi, kubainisha semi zilizoandikwa katika mabango ya biashara, pili, kuonyesha mbinu za kisanaa zinazotumika wakati wa uandishi wa semi na tatu, kujadili dhamira na athari za semi zilizoandikwa katika mabango hayo. Data za utafiti huu zimekusanywa kutoka maktabani na uwandani ambapo data za maktabani zimekusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji maandiko na data za uwandani zimekusanywa kwa kutumia mbinu tatu za ukusanyaji data. Mbinu hizo ni Ushuhudiaji, majadiliano na hojaji. Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji na Nadharia ya Sosholojia zimetumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data za utafiti huu. Utafiti huu umebaini kuwa kuna semi mbalimbali katika mabango ya biashara ambazo tumezigawa zenye kuakisi fitina na majungu, imani juu ya Mungu, mila na utamaduni, uchumi na subira na uvumulivu. Aidha, utafiti umeona kuwa katika uandishi wa mabango ya biashara kuna mbinu kuu tatu ambazo hutawala uandishi. Mbinu hizo ni kama vile lugha, muundo na mtindo. Halikadhalika, utafiti umegundua kwamba dhamira kuu za waandishi wa semi ni kuonyesha hali zinazowatokea katika jamii zao kama vile, fitina na majungu, imani juu ya Mungu, mila na utamaduni, uchumi na subira na uvumulivu ambapo hata athari za semi hutokana na hali hiyo. Kwa ujumla, utafiti huu umetoa mwanzo wa kubainisha semi na dhamira zake katika mabango ya biashara.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Sep 2018 08:41
Last Modified: 30 Sep 2018 08:41
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2007

Actions (login required)

View Item View Item