Kuchunguza Fani na Dhamira ya Malezi ya Watoto katika Riwaya ya Kiswahili: Mfano Watoto wa Mama N’tilie

Othman, Zaina Omar (2018) Kuchunguza Fani na Dhamira ya Malezi ya Watoto katika Riwaya ya Kiswahili: Mfano Watoto wa Mama N’tilie. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of ZAINA OMAR OTHMAN FINAL-TASNIFU-13-02-2018.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (1MB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unahusu: Kuchunguza Fani na Dhamira ya Malezi ya Watoto katika Riwaya ya Kiswahili: Mfano Riwaya ya Watoto wa Mama N’tilie. Utafiti ulikuwa na malengo mahsusi mawili, ambayo ni: Kubainisha mbinu za kisanaa zilizotumika katika kujenga dhamira ya malezi ya watoto katika riwaya ya Watoto wa Mama N’tilie na lengo la pili ni kuchambua dhamira ya malezi ya watoto katika riwaya ya Watoto wa Mama N’tilie. Katika kutimiza malengo haya, mtafiti alikusanya data kwa kutumia mbinu za usomaji makini na upitiaji wa nyaraka maktabani na kufanya uchambuzi wa data kwa kutumia mbinu ya mkabala wa kimaelezo na nadharia ya Simiotiki na Sosholojia. Matokeo ya utafiti yameonesha kwamba, suala zima la malezi ya watoto ni changamoto kwa wazazi na jamii. Kwa lengo la kupatikana ufanisi wa malezi na maadili mema ni lazima pande mbili za familia zishirikiane kwa pamoja ili kujenga familia bora. Kwa ujumla ni matumaini ya mtafiti kufikisha vyema dhamira ya malezi na kuamsha ari kwa jamii na taifa kwa ujumla na kupelekea kushajihishika kuwalea watoto wetu katika maadili mema kwa faida ya familia, jamii na taifa kwa lengo la kuwa na taifa bora la baadae.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Sep 2018 08:33
Last Modified: 30 Sep 2018 08:33
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2006

Actions (login required)

View Item View Item