Tathmini ya Mitaala ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Nchini Tanzania Imuandaavyo Mwanafunzi Kumudu Somo la Isimu Chuo Kikuu

Luziga, Ndijenyene Braisony (2017) Tathmini ya Mitaala ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari Nchini Tanzania Imuandaavyo Mwanafunzi Kumudu Somo la Isimu Chuo Kikuu. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of TASINIFU YA LUZIGA-09-10-2017.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (1MB) | Preview

Abstract

Azma ya utafiti huu, ilikuwa ni kuchunguza jinsi mtaala wa elimu ya sekondari nchini Tanzania kwa mada zinazohusiana na isimu katika somo la Kiswahili zinavyomuwezesha mwanafunzi anayehitimu kidato cha sita kusoma somo la isimu vyuo vikuu. Utafiti ulikusudia kuchunguza mada zenye msaada zaidi na zile zisizokuwa na msaada kwa mwanafunzi atakayekwenda kusoma isimu Chuo Kikuu. Aidha utafiti ulikusudia pia kuchunguza maoni ya walimu kuhusu mada za isimu katika somo la Kiswahili katika shule za Sekondari. Mwisho kabisa utafiti ulikusudia kubaini mbinu zinazoweza kutumika ili kupunguza au kuondoa mapungufu ambayo yatakuwa yamebainishwa katika malengo mahususi yaliyotajwa hapo juu. Utafiti huu umefanyika mkoani Tabora katika Manispaa ya Tabora. Jumla ya shule za sekondari saba zimeshirikishwa. Pia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha AMUCTA wameshirikishwa katika utafiti huu. Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu zilikuwa ni hojaji, mahojiano na Maktabani. Data zimechanganuliwa kwa mbinu ya kiidadi na isiyo ya kiidadi. Utafiti umeongozwa na nadharia ya uamilifu. Matokeo ya utafiti huu yamebaini kwamba; zipo mada za isimu katika somo la Kiswahili za sekondari ambazo humuandaa vema mwanafunzi wa Kiswahili sekondari atakayekwenda kusoma somo la isimu vyuo vikuu. Kwa upande wa pili; kwanza, imebainika kuwa zipo baadhi ya mada na sehemu za mada ambazo haziwaandai vema wanafunzi watakaokwenda kusoma isimu vyuo vikuu, tatu utafiti umebaini kuwa walimu wa somo la Kiswahili na wanafunzi wana maoni hasi kuhusiana na mada za isimu na isimu kwa ujumla. Na nne, utafiti huu umebaini kuwa kuna njia kadhaa zinazoweza kutumika ili kupunguza au kuondoa mapungufu yaliyobainishwa katika utafiti huu.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 30 Sep 2018 08:04
Last Modified: 30 Sep 2018 08:04
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/2000

Actions (login required)

View Item View Item