Amanyisye, Kibungu Timothy
(2017)
Kuchunguza Dhima ya Nyimbo kwa Wafiwa Katika Jamii ya Wanyakyusa Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Masters thesis, The Open University of Tanzania.
Abstract
Lengo kuu la utafiti wetu lilikuwa kuchunguza dhima ya nyimbo kwa wafiwa katika jamii ya Wanyakyusa wa Kata ya Lufingo, kijiji cha Ighembe (Kalalo), Itete, Kagwina, na Simike, wilaya ya Rungwe, mkoa wa Mbeya. Malengo mahususi yalikuwa ni kubainisha dhima za nyimbo za msiba kwa wafiwa wa jamii ya Wanyakyusa, Kuchambua dhamira katika nyimbo za msiba za jamii ya Wanyakyusa na kuelezea uhalisia wa nyimbo hizo kwa jamii ya leo. Data za utafiti zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usaili na ushiriki na kuchambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa kimaelezo na nadharia ya Saikolojia Changanuzi. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa nyimbo hizo zina dhima ya kuelimisha, kukosoa jamii, kuliwaza, kuhimiza watu kufanya mambo mema na kutunza mila na dasturi za jamii. Kwa upande wa dhamira zimekuwepo dhamira za malezi mema, kifo, kumuombea marehemu, kutoogapa kifo na kumuogopa Mwenyezi Mungu. Kwa jumla dhamira hizi zina uhalisia katika maisha ya kila siku ya jamii kwani kila mtu ataonja umauti na hivyo ni vizuri kufanya matendo mazuri ili kuweza kuishi vizuri katika kipindi chote cha uhai wa mtu hapa duniani
Actions (login required)
|
View Item |