Uchambuzi linganishi wa Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiunguja Mjinikama Lahaja za Kiswahili

Ameir, Salma Abdalla (2018) Uchambuzi linganishi wa Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiunguja Mjinikama Lahaja za Kiswahili. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of SALMA  ABDALLA  AMEIR TASNIFU.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (634kB) | Preview

Abstract

Lengokuu la utafiti ni Uchambuzi linganishi wa Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiunguja mjini kama lahaja za Kiswahili. Malengo ya utafiti yalikuwa ni: Kuorodhesha na kulinganisha msamiati wa Kimakunduchi, Kitumbatuna Kiunguja mjini. Kufananisha Kiunguja mjini, Kitumbatu na Kimakunduchi. Kutofautisha Kiunguja mjini na Kitumbatu na Kimakunduchi na mwisho Kuonyesha uhusiano wa lahaja za Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiunguja mjini. Ili kufikia lengokuu lililokusudiwa mbinu mbalimbali za utafiti zilihusika, ambazo ni mahojiano na dodoso. Nadharia mbili zilizoongoza utafiti huu ni nadharia ya Makutano na mwachano ya Giles (1982).Sampuli iliyotumika ni watu 45, Tumbatu watukumi na tano,Makunduchi watukumi na tano na Mjini watu kumi na tano. Kwa upande wa matokeo ya utafiti, mtafiti aligunduakuwa msamiati wa Kiunguja mjini na Kimakunduchi unafanana zaidi kuliko Kitumbatu. Maneno 370 yanaonyesha kufanana kati ya Kimakunduchi na Kitumbatu, ambayo sawa na asilimia 74, na kutofautiana kwa maneno 130 sawa na asilimia 26. Hali hii inaonyesha kuwa Kimakunduchi kimekopa maneno mengi katika lahaja ya Kiunguja kwa lengo la kupata kuongeza msamiati wa lahaja yao kwa mawasiliano baina yao. Kitumbatu na Kimakunduchi zinafanana kwa maneno 296 sawa asilimia 59.2na kutofautiana kwa maneno 204sawa na asilimia 40.8. Kiunguja mjini na Kitumbatu lahajahizi zinafanana kwa maneno 286 sawa na asilimia 57.2 na kutofautiana kwa maneno 214 sawana asilimia 42.8. Kufanana kwa Kiunguja mjini na Kimakunduchi imebainika kuwa lahajahizi zipo katika kisiwa cha Unguja na tofauti kati ya Kitumbatu na Kiunguja mjini ni ile ya kuwa Kitumbatu kinazungumzwa katika kisiwa cha Tumbatuhivyo tunaona kuwa Kiunguja na Kitumbatu kinatokana na Visiwa tofauti lakinizote zikiwa ni miongoni mwa lahaja za Kiswahili, hali hii imebainika baada yakufanyika uchambuzi wa kina wa lahaja hizi.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 29 Sep 2018 13:06
Last Modified: 29 Sep 2018 13:06
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1993

Actions (login required)

View Item View Item