Kuchunguza jinsi Nahau za Kiswahili Sanifu Zinavyokwamisha Mawasiliano Fanisi kwa Wageni wa Lugha

Skuni, Mwanaisha Mussa (2018) Kuchunguza jinsi Nahau za Kiswahili Sanifu Zinavyokwamisha Mawasiliano Fanisi kwa Wageni wa Lugha. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Mwanaisha Mussa Skuni-TASNIFU-13-02-2018.pdf]
Preview
PDF - Submitted Version
Download (900kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu unalenga“Kuchunguza jinsi Nahau za Kiswahili zinavyokwamisha Mawasiliano kwa Wageni wa Lugha”. Nahau hizo zinatumika katika lugha ya maandishi ya Kiswahili na katika mazungumzo ya kila siku. Mtafiti wa utafiti huu aliongozwa na malengo mahsusi matatu ambayo ni kubainisha nahau mbali mbali za lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia makundi yake kimuktadha, kuchambua maana ya nahau Kipragmatiki na maana ya nahau kwa kuzingatia viambajengo vilivyounda nahau hizo (Kisemantiki), na kubainisha jinsi nahau zinavyokwamisha mawasiliano kwa wageni wa lugha. Utafiti huu umefanyika katika kisiwa cha Pemba, katika hospitali ya Wete,hopitali ya wakorea Chake chake na hospitali ya Abdalla Mzee na katika Mtaa wa Mkoroshoni Chake chake. Pia utafiti hu ulifanyika shule ya sekondari ya Uweleni na shule ya sekondari ya Utaani na Chuo Cha Kiislamu Pemba Mbinu ya uwandani na maktabani zilitumika katika kufanya utafiti huu na njia zilizotumika ni dodoso, mahojiano . Sampuli iliyotumika ni ya wanafunzi na walimu wa somo la Kiswahili wa shule zilizoteuliwa. Mtafiti alitumia nadharia ya maana katika matumizi na nadharia ya maana katika muktadha. Matokeo ya jumla ya utafiti huu yanaonyesha kuwa lugha ya kiswahili ni pana katika matumizi yake. Pia mtafiti amegundua kuwa mambo yanayopelekea matumizi ya nahau yasababishe kufeli kwa mawasiliano kwa wageni wa lugha ni pamoja na wageni kujifunza zaidi sarufi ya lugha na kuiwacha kabisa kabisa fasihi ya lugha.Vile vile Nahau hazitoi maana kisarufi. Hata hiyo matokeo yanaonyesha kuwa nahau hazikwamishi mawasiliano kwa wageni wa lugha tu bali pia na wazawa wa lugha wanakabiliwa na taizo hili.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 29 Sep 2018 12:05
Last Modified: 29 Sep 2018 12:05
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1980

Actions (login required)

View Item View Item