Mtazamo wa Jamii Juu ya Sera ya Elimu na Mafunzo 2014 Kuhusu Kutumia Kiswahili Kufundishia na Kujifunzia Elimu ya Juu katika Vyuo vya Kati

Ambrose, Vedastus L. G. (2018) Mtazamo wa Jamii Juu ya Sera ya Elimu na Mafunzo 2014 Kuhusu Kutumia Kiswahili Kufundishia na Kujifunzia Elimu ya Juu katika Vyuo vya Kati. Masters thesis, The Open University of Tanzania.

[thumbnail of Ambrose-TASNIFU-31-01-2018.pdf]
Preview
PDF
Download (805kB) | Preview

Abstract

Utafiti huu ulilengakuchunguza mtazamo wa jamii juu ya Sera ya Elimu na Mafunzo 2014 kuhusu matumizi ya Kiswahili katika kufundishia na kujifunzia katika vyuo vya kati. Utafiti huu ulikuwa na madhumuni mahsusi matatu ambayo ni kubaini tamko la sera ya elimu kuhusu matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia, Kubainisha changamoto za utekelezaji wa sera ya Elimu kuhusu matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia, Kutoa mapendekezo juu ya utekelezaji wa sera ya elimu kuhusu matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia.Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya kijamii na utekelezaji. Utafiti huu ulifanywa katika wilaya za Nyamaganana Ilemela katika vyuo vya CBE na ADEM kwa kutumia watafitiwa 95 waliosailiwa na kujibu maswali. Watafitiwa waliteuliwa kwa kuzingatia kigezo cha nasibu na makusudi.Mbinu ya utafiti iliyotumika katika kukusanya data ilikuwa ni usaili, hojaji na utalii wa machapishi.Uchambuzi wa data zilizokusanywa umefanyika kwa kutumia mkabala wa kimaelezo na kitakwimu.Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa lugha ya Kiswahili inakidhi vigezo vyote vya kutumika kama lugha ya kufundishia na kujifunzia elimu katika vyuo vya kati. Matumizi ya lugha inayotumiwa na wazungumzaji wengi inaweza kuwa ni nyenzo muhimu katika kuinua ubora wa elimu itolewayo katika vyuo hivyo. Kutotumika kwa lugha ya Kiswahili kufundishia elimu nchini Tanzania hakuwasaidii wanafunzi kufikia viwango vinavyotakiwa. Aidha, hakusaidii kuendeleza vipaji na ubunifu wa wanafunzi katika kuikuza lugha ya Kiswahili ili iendane na mahitaji ya kutumika kufundishia na kujifunzia elimu ya kati.

Item Type: Thesis (Masters)
Subjects: 400 Language > 490 Other languages
Divisions: Faculty of Arts and Social Sciences > Department of Linguistics and Literary Studies
Depositing User: Mr Habibu Kazimzuri
Date Deposited: 27 Sep 2018 07:04
Last Modified: 27 Sep 2018 07:04
URI: http://repository.out.ac.tz/id/eprint/1905

Actions (login required)

View Item View Item